Mahsa Amini

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Mahsa Amini alikuwa mwanamke kijana ambaye aliuawa na serikali ya Iran. Kifo chake kilisababisha maandamano makubwa nchini Iran na duniani kote.

Maisha[hariri | hariri chanzo]

Machafuko nchini Ujerumani

Mahsa Amini alizaliwa tarehe 21 Septemba mwaka wa 2000. Yeye alizaliwa katika jiji la Saqqez, jimbo la Kurdistan, nchi ya Iran. Jina lake la Kiajemi lilikuwa Mahsa, lakini jina lake la Kikurdi lilikuwa Jina au Zhina. Yeye alikuwa na kaka mmoja mdogo. Baba yake alikuwa mfanyakazi wa serikali na mama yake hakuwa na kazi. Mahsa alikwenda Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Talegheni katika jiji la Saqqez na alihitimu mwaka wa elfu mbili kumi na nane. Wakati wa kifo chake, Mahsa Amini alikubaliwa katika chuo kikuu nchini Iran na alitaka kuwa mwanasheria. Kabla ya kifo chake, Mahsa hakujihusisha na siasa na yeye alikuwa na afya njema na hakuwa na hali mbaya zozote za kiafya. Kwa bahati mbaya, aliuawa na serikali ya Iran akiwa na umri wa miaka ishirini na mmoja.[1]

Kifo[hariri | hariri chanzo]

Mwanamke anayekata nywele zake kupinga sheria za lazima za hijabu

Mwezi Septemba mwaka 2022 Mahsa alikwenda jijini Tehran kumtembelea kaka yake. Katika tarehe kumi na tatu, mwezi wa Septemba, yeye alikamatwa na Polisi wa Maadili wa Iran katika jiji la Tehran kwa sababu hakuwa amevaa hijabu yake ipasavyo na alikuwa amevaa mavazi ‘yasiyo ya heshima’. Wakati wa kukamatwa kwake, Mahsa aliteswa na kupigwa na polisi. Alipoteza fahamu na baada ya siku chache, yeye alifariki. Polisi wa Iran walisema kuwa wao hawakumtesa na hawakumpiga Mahsa. Pia, wao walisema kuwa yeye alifariki kwa sababu ya tatizo la moyo. Hata hivyo, watu wengi waliona polisi wa Iran wakimpiga na walisikia polisi wakimtukana na kumlaani. Pia, familia yake ilisema kuwa yeye alikuwa na afya njema na hakuwa na matatizo yoyote ya kiafya.[2] Hospitali ambapo Amina alifarikia ilisema kuwa alikuwa amekufa kwa sababu polisi walimuumiza sana kichwani. Serikali ya Iran inajaribu kuficha ukweli wa kifo cha Mahsa.[1]

Machafuko nchini Iran[hariri | hariri chanzo]

Kifo cha Mahsa Amini kilisababisha maandamano na machafuko dhidi ya serikali ya Iran. Maandamano na machafuko yalianza masaa machache baada ya kifo chake. Wairani waliimba “mwanamke, maisha, uhuru” mitaani. Pia, wanawake wengi walikata nywele zao kupinga sheria za lazima za hijabu.[3] Sasa, watu duniani kote wanasambaza kisa cha Mahsa Amini kwenye mitandao ya kijamii. Lakini, vyombo vya habari vya Irani na vyombo vya habari katika nchi zingine havionyeshi maandamano na vifo vya Wairani mikononi mwa polisi. Wanawake wengi duniani kote na Wairani wanapigania uhuru wao na maisha yao.[4]

Mwitikio wa Serikali ya Iran[hariri | hariri chanzo]

Polisi wa Iran

Kwa sababu ya machafuko nchini Iran, serikali ya Iran ilifunga intaneti na kuzuia matumizi ya mitandao ya kijamii. Serikali ilitumia mabomu ya machozi na bunduki dhidi ya waandamanaji ambayo yaliua na kujeruhi Wairani wengi. Tarehe nne, mwezi wa Disemba, mwaka wa elfu mbili ishirini na mbili, Polisi wa Maadili nchini Iran wamefutwa na serikali ya Iran inafanya mikakati kubadilisha sheria za hijabu. [3]

Historia ya Kuvaa Hijabu nchini Iran[hariri | hariri chanzo]

Nukuu imeandiwa kwenye kaburi lake "Mpendwa Zina, hutakufa. Jina lako litakuwa mwito wa maandamo"

Baada ya Mapinduzi ya Iran mwaka 1979, serikali ya Iran ilianzisha kanuni ya lazima ya mavazi kwa wanawake. Serikali ilisema kuwa wanawake walihitaji kuvaa hijabu katika mahali pao pa kazi. Baada ya sheria hii, kulikuwa na ukatili dhidi ya wanawake ambao hawakuvaa hijabu ipasavyo. Katika mwaka 1983 , wanawake walihitajika kuvaa hijabu wakati ambapo walikwenda nje ya nyumba zao. Ikiwa hawakuvaa hijabu, wangechapwa viboko au kufungwa jela.[1] Katika miaka kumi iliyopita, wanawake vijana walikua huru zaidi kuhusu sheria na mavazi ya hijabu. Kwa hivyo, Polisi wa Maadili waliwaleta wanawake kwenye vituo ili “kuwafundisha tena” kuhusu mavazi na sheria za hijabu. Machafuko na maandamano yametokea tangu Mapinduzi ya Iran mwaka elfu moja mia tisa sabini na tisa, lakini sasa machafuko haya yamekuwa makali zaidi.[5]

Kifo cha Mahsa Amini kilisababisha upinzani wa wanawake na Wairani dhidi ya serikali ya Iran kwa sababu wao wanataka uhuru. Nukuu imeandikwa kwenye kaburi lake: ژینا گیان تۆ نامری. ناوت ئەبێتە ڕەمز / “Beloved Zina [Mahsa], you will not die. Your name will become a rallying call” / “Mpendwa Zina [Mahsa], hutakufa. Jina lako litakuwa mwito wa maandamano.” [1]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. 1.0 1.1 1.2 1.3 "Death of Mahsa Amini", Wikipedia (in English), 2022-12-11, retrieved 2022-12-11 
  2. Machafuko Iran: Wanawake wachoma hijabu kwenye maandamano ya kupinga sheria za hijabu (sw). BBC News Swahili (2022-09-21). Iliwekwa mnamo 2022-12-11.
  3. 3.0 3.1 Waandamanaji Iran: 'Walisema tusiponyamaza watatubaka' (sw). BBC News Swahili (2022-09-28). Iliwekwa mnamo 2022-12-11.
  4. Sullivan, Becky; Kenyon, Peter (2022-11-29), "The U.S.-Iran World Cup matchup puts a spotlight on Iran's protest movement", NPR (in English), retrieved 2022-12-11 
  5. Iran general acknowledges more than 300 people have been killed in protests sparked by death of Mahsa Amini (en-US). www.cbsnews.com. Iliwekwa mnamo 2022-12-11.