Magda al-Sabahi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Magda Sabbahi
[[Image:Magda 2|frameless]]
Amezaliwa Misri
6 Mei 1931
Amekufa 16 Januari 2020
kairo, Misri
Jina lingine Magda
Kazi yake Mwigizaji, mtayarishaji
Miaka ya kazi 1949 – 1994


Magda Sabbahi au Magda (kwa Kiarabu ماجدة) ; 6 Mei 193116 Januari 2020) alikuwa mwigizaji wa nchini Misri akianza kujulikana kunako mwaka 1949 hadi 1994.

Maisha[hariri | hariri chanzo]

Afaf Ali Kamel Sabbahi alizaliwa mwezi Mei mwaka 1931 huko Tanta. alikuwa ni mmoja wa nyota maarufu zaidi wa Filamu nchini Misri akiwa amecheza zaidi ya filamu sitini na katika taaluma yake ya filamu alipenda kujiita Magda. Mwaka 1956, Magda alianzisha kampuni yake ya utengenezaji wa filamu na mwaka 1958 aliigiza katika filamu ya Djamila Bouhired. Mwaka 1963,aliolewa na ofisa usalama na muigizaji Ihab Nafe,na kujaliwa kupata mtoto wa kike, mwaka 1965 .[1]

Kifo[hariri | hariri chanzo]

Magda Sabbahi alifariki nyumbani kwake katika mji mkuu wa Kairo mwaka 2020 akiwa na umri wa miaka 88[2]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mwigizaji filamu fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Magda al-Sabahi kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.