Maeneo ya hifadhi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Maeneo ya hifadhi[1] ni maeneo yanayopata ulinzi kwa sababu ya maadili yanayotambulika ya asili, kiikolojia au kitamaduni.

Kuna aina kadhaa za maeneo yaliyohifadhiwa, ambayo hutofautiana kwa kiwango cha ulinzi kulingana na sheria wezeshi za kila nchi au kanuni za mashirika ya kimataifa yanayohusika. Ingawa kwa ujumla, maeneo yaliyohifadhiwa yanaeleweka kuwa yale ambayo uwepo wa binadamu au angalau unyonyaji wa maliasili ni mdogo.

Nchi nyingi sasa zimetenga maeneo makubwa kuwa mbuga za wanyama, mapori ya akiba, au hifadhi za misitu. Kati ya mbuga hizi, ni baadhi tu ambazo ni kubwa vya kutosha kuwa na mifumo ya ikolojia inayojitosheleza, na nyingi zimetengwa ili kubeba mamalia wakubwa.

Katika Afrika ya Mashariki pia kuna hifadhi za ndege na viumbe vya baharini. Uhifadhi wa uoto unafanywa hasa katika hifadhi za misitu lakini pia katika hifadhi ya taifa. Kwa kuongezea, nchi kadhaa zinajaribu kuhifadhi wanyamapori kwa kukataa leseni za kuuza nje aina fulani za ngozi, haswa zile za chui, duma na punda milia.

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mambo ya biolojia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Maeneo ya hifadhi kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.