Maduka ya United Cigar Stores

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
United Cigar Stores
Jina la kampuni United Cigar Stores
Ilianzishwa 1901
Huduma zinazowasilishwa Uuzaji wa sigara na bidhaa mbalimbali
Nchi MarekaniMarekani
Mnamo 1917-04-19 jengo la Flatiron Building United Cigar Store lilibadilishwa kuwa jumba la sherehe ya "Wake up America Day"
United Cigar Stores inafurahia sheria mpya ya 1918 ya ufanyikazi

Historia[hariri | hariri chanzo]

United Cigar Stores ilikuwa mnyororo mkubwa kabisa wa maduka ya sigara huko Marekani. Ingawa mwanzoni maduka haya yalikuwa ya kuuza sigara tu,walianza kuuza bidhaa nyingine mbalimbali,kama saa za aina ya Mickey Mouse na viatu. Mnyororo huu wa maduka ulianzishwa katika mwaka wa 1901. [3] Ingawa wengi walikana,mnyororo huu uliwakilisha maslahi ya kampuni ya Consolidated Tobacco Company, hii ilikuwa shirika la tumbaku lililosimamia kampuni zingine za tumbaku kama American Tobacco Company na zinginezo. Mnamo Septemba 1903, mkataba uliundwa na washindani wa mnyororo huo na huu ukafanya mnyororo huo kutokuwa na upinzani au ushindani wowote katika biashara yao. Ulipofika mwaka wa 1926,mnyororo huo ulikuwa na maduka takriban 3000 ya rejareja.

Kampuni hii iliongozwa na Whelan-Schulte lakini usimamizi ukaenda kwa George Kenan na Frederick Morrow katika mwezi wa Agosti 1929. Kampuni hii ,pia, ilikuwa imejihusisha katika biashara ya mali isiyohamishika. Shida za kiuchumi zilipopata Marekani katika miaka ya 1929 na mwanzoni mwa miaka ya 1930,sehemu ya mali isiyohamishika ilileta hasara kubwa.HIvyo basi,katika mwezi wa Septemba 1932 kampuni yenyewe ikatangaza kuwa haina pesa. Kabla ya kuwa fukara, kampuni hii ilikuwa na maduka 975 ya sigara na maduka 219 ya dawa,lakini mali yake nyingi ilikuwa mali isiyohamishika. Mnyororo ulinawiri tena na ukawa umefungua maduka 1300 kablla ya mwaka wa 1951 kuisha.

United Cigar Stores ikawa sehemu ya Shirika la United Cigar-Whelan Stores lililobadilika likawa Shirika la United Whelan:katika miaka ya 1960 iliungana na Shirika la Perfect Film & Chemical,kampuni ya kusindika filamu na kuuza dawa na vitamini. Perfect Film & Chemical ilibadilisha jina ikawa Cadence Industries katika mwaka wa 1973.Labda,sehemu yake maaarufu kabisa ni Marvel Comics, ilimiliki Marvel tangu 1968 hadi 1986.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. ^ Schulte & Specialties. 1937-11-29.
  2. ^ Milestones. 1941-12-22.
  3. ^ John Moody. The Truth About The Trusts: A Description and Analysis of the American Trust Movement. New York: Moody Publishing; 1904. OCLC 1832950. Consolidated Tobacco Company and affiliated corporations. 'The Tobacco Trust.' p. 69–96ff.
  4. ^ Salesmen. 1926-12-20.
  5. ^ Two Morrows. 1929-09-02.
  6. ^ Cigar Stores. 1932-09-05.
  7. ^ United Cigar. 1951-10-15.
  8. ^ New Man for Curtis. 1968-05-03.

Kwa masomo zaidi[hariri | hariri chanzo]