Madiha Abdalla

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Madiah Abdalla[1] ni mwandishi wa habari wa Sudan na mhariri mkuu wa kwanza mwanamke wa gazeti la Sudan El Meidan tangu mwaka 2011, lililloko chini ya Chama cha Kikomunisti cha Sudan. Madiah ni miongoni mwa wanawake waanzilishi katika uandishi wa habari akifuatia hatua za wanaharakati wa haki za wanawake, kama vile Fatima Ahmed Ibrahim mnamo mwanzoni miaka ya 1940, ambaye alitoa gazeti la Women's voice.

Kazi[hariri | hariri chanzo]

Abdalla alianza taaluma yake kama mwanahabari katika gazeti la El Meidan mnamo 1985. Kisha alifanya kazi katika magazeti tofauti, kama vile Alayam. Abdalla pia aliandika idadi ya safu katika El Meidan baada ya Mkataba Kabambe wa Amani CPA nchini Sudan.

Abdalla ambaye ni mwanaharakati wahaki za wanawake, anatoa wito wa usawa wa wanawake na anajitahidi kupunguza ubaguzi wa kijinsia kama pengo mojawapo nchini Sudan. Ameandika makala kuhusu masuala ya wanawake katika kurasa tofauti za mtandaoni, kama vile katika jukwaa maarufu Sudaneseonline.

Kukamatwa na kesi mahakamani[hariri | hariri chanzo]

Kutokana na maandishi yake, Abdalla amekuwa kizuizini na akakabiliwa na kesi mwezi wa Aprili 2017. Katika kesi nyingine mwaka wa 2014, ambapo Abdalla alikabiliwa na shutuma za Huduma ya Kitaifa ya Ujasusi na Usalama ya Sudan (NISS) ambapo alipatikana na hatia ya kuchapisha habari za uongo.[2]

Marejeleo[hariri | hariri chanzo]