Mad Ice

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Pitio kulingana na tarehe 00:12, 15 Februari 2013 na Rich Farmbrough (majadiliano | michango) (Minor fix using AWB)

Ahmed Mohamed Kakoyi

Mwanamuziki Mad Ice.
Mwanamuziki Mad Ice.
Jina Kamili {{{jina kamili}}}
Jina la kisanii Mad Ice
Nchi Muuganda, Mtanzania
Alizaliwa 8 Oktoba 1980
Aina ya muziki Raga Mafin, Bongo Flava
Kazi yake Muimbaji
Miaka ya kazi mn. 1998 hadi 2007
Ameshirikiana na Mike T, Sugu
Ala sauti
Kampuni Mwamba Records Finland

Ahmed Mohamed Kakoyi au ( Mad Ice ) ni mwanamzuki wa 'Raga Mufin' nchini Uganda-Tanzania. Mad Ice amezaliwa tar. 8 Oktoba ya mwaka wa 1980 nchini Uganda, na kukulia katika mji wa Mwanza, Tanzania.

Mad Ice ambae ni Mganda anae fanya shughuli zake za kimuziki nchini Tanzania, amejibebea umaarufu mkubwa nchini Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla.

Mad Ice ambaye kwa sasa anaishi nchini Finland kwasababu ya shughuli za kimuziki.

Safari ya Finland

Uwezo wake katika sanaa ulimvutia prodyuza wake Miikka Mwamba, raia wa Finland aliye wahi kuweka makazi yake nchini Tanzania. Na wakati mkataba wake katika studio ya FM ulipomalizika, Miikka alirejea kwao na ndipo alipomualika Mad Ice Ulaya kwa mara ya kwanza. Hiyo ilikuwa mwaka 2004 wakati Miikka alipomualika Mad Ice Finland. Alimualika kwa ajili ya kumfanyia promosheni albam yake ya `Baby Gal` katika soko la Ulaya.

mwaliko wake wa kwanza ulizaa matunda alifanya vizuri jambo lililopelekea aalikwe tena na tena katika matamasha mbalimbali makubwa ya nchini hapo na hata Sweden,

Ushirkiano wake na Prodyuza Miikka Mwamba

Mad Ice Akiwa Jukwaani

Ushirikiano wake na Miikka nchini Finland ukaleta matunda mapya mwaka 2005 wakati alipokamilisha albam yake ya pili aliyoiita `Mad Ice` na kuitawanya katika soko la Ulaya huku ikiuzwa pia kupitia tovuti yake.

Albam hiyo iliyosambazwa na lebo ya Edel Records ya Finland, ilijumuisha pia wimbo uliomtoa Mad Ice wa `Baby Gal` uliokuwemo katika albam yake ya kwanza yenye jina hilo aliyoitoa Afrika Mashariki mwaka 2003.

Agosti 2005 Mad Ice akaachia single mpya ya `Wange` Afrika Mashariki iliyomrejesha katika chati za muziki wa kizazi kipya. wimbo wake ambao aliuimba nchini Finland ulirushwa kwa mara ya kwanza Agosti 15 kupitia kituo cha radio cha huko cha Power FM, aliuimba akizungumzia upendo wake kwa mkewe mzungu aliyezaa naye mtoto mmoja wa kiume.

Maisha Binafsi

Mad Ice alikutana na mwanamke Mzungu amabaye ni raia wa Finland na kufunga naye ndoa huko huko nchini Finland, Mad Ice sasa ana mke na Mtoto Mmoja na pia Mad Ice ana watoto wengine wawili aliowapata katika mahusiano yake yaliyopita, Wa kwanza ana miaka saba allimpata akiwa shule ya sekondari nchini Uganda na wa pili ana miaka mitatu... huyo alimpata nchini Tanzania, kama unavyojua tena vijana wanakuwa na mambo mengi, lakini baadaye akamua kuoa, msanii huyu Mad Ice aliyeweka kambi yake nchini Finland.

Nyimbo Zenye Umaarufu

  • 1 Wanadamu
  • 2 Baby Gal
  • 3 Wange
  • 4 Ni Wewe

Tovuti Binafsi

Tovuti Binafsi ya Mad Ice