Nenda kwa yaliyomo

Tokeeo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Macronyx)
Tokeeo
Tokeeo koo-njano
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Ngeli: Aves (Ndege)
Oda: Passeriformes (Ndege kama shomoro)
Familia ya juu: Passeroidea (Ndege kama shomoro)
Familia: Motacillidae (Ndege walio na mnasaba na matikisa)
Horsfield, 1821
Ngazi za chini

Jenasi 2, spishi 9:

Tokeeo ni ndege wa jenasi Macronyx na Tmetothylacus katika familia ya Motacillidae. Wanafanana na matikisa lakini tokeeo ni wakubwa zaidi na makucha ya nyuma ni marefu sana, marefu hata kuliko yale ya vipimanjia. Mgongo wao una michirizi kahawia na wana rangi ya manjano, machungwa au nyekundu chini. Wana mkufu mweusi kidarini. Ndege hawa wanatokea Afrika tu na hupatikana ardhini; hula wadudu. Tago lao ni kikombe cha manyasi ardhini na jike huyataga mayai 2-4.