Sukulenti : Tofauti kati ya masahihisho
Ukurasa ulianzishwa kwa kuandika '300px|thumbnail|Jani la Aloe lililokatwa; utomvu unatoka nje '''Sukulenti''' (lat. ''sucus'' = utomvu; ing. ''succulents'') au...' |
(Hakuna tofauti)
|
Pitio la 10:14, 1 Desemba 2014
Sukulenti (lat. sucus = utomvu; ing. succulents) au Mimea wenye utomvu mwingi ni mimea iliyojitohoa kwa maisha katika mazingira yabisi.
Mimea hii ya familia na jenasi tofauti ina uwezo wa kutunza maji ndani ya majani au mashina yao. Kwa hiyo mara nyingi ama majani au shina ni nono kutokana na uwingi wa utomvu ndani yao.
Kwa hiyo "sukulenti" si jina la spishi au familia maalumu ya mimea lakini inataja umbo la mmea unaotkuwa tofauti kutokana na mazingira. Mimea ya aina (jenasi) moja inaweza kupatikana kwa majani nono yenye utomvu mwingi au kwa majani ya kawaida yakikua katika mazingira tofauti.
Pia kuna tofauti kati ya watalaamu eti ni nini inayostahili kuitwa sukulenti. Wengi wanaangalia majani na mashina pekee lakini kuna wengine wanaoingiza mle pia mizizi inayotunza maji lakini wengine hawakubali.
Mifano ya sukulenti iliyokubalika na pande zote ni mbuyu, mkonge, aloe vera na aina za mpungate.
-
Mkonge hupandwa kwa mashamba makubwa katika nchi yabisi ikihifadhi maji kwenye majani yake
-
Mbuyu wa Madagaska hutunza maji katika shina lake
-
Mipungate inatoa maua mazuri inapendwa kama mimea ya mapambo
-
Mpungate unapaswa kujilinda kwa miiba kwa kutunza maji ndani yake dhidi ya wanyama wa jangwani wenye kiuu
Makala Biolojia bado ni mbegu. Unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuongezea habari. |