Dolar ya Marekani : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
d r2.6.4) (roboti Nyongeza: rue:США долар
d r2.6.2) (roboti Nyongeza: tk:Dollar
Mstari 115: Mstari 115:
[[tg:Доллари ИМА]]
[[tg:Доллари ИМА]]
[[th:ดอลลาร์สหรัฐ]]
[[th:ดอลลาร์สหรัฐ]]
[[tk:Dollar]]
[[tl:Dolyar ng Estados Unidos]]
[[tl:Dolyar ng Estados Unidos]]
[[tr:ABD doları]]
[[tr:ABD doları]]

Pitio la 23:55, 22 Julai 2011

Dola ya Marekani

Dola ya Marekani (US-Dollar, kifupi USD) ni pesa halali ya Marekani. Alama yake ni USD au mara nyingi alama ya dola tu $.

Dola ya Marekani inapatikana kwa benknoti za dola 1, 2, 5, 10, 20, 50 na 100. Kuna pia sarafu ya dola 1.

Dola moja ina senti 100. Senti huitwa pia "penny" nchini Marekani. Kuna sarafu za nusu dola (half dollar, senti 50), robo dola (quarter, senti 25) na sarafu za senti 10 (dime), 5 (nickel) na 1 (penny).

Hadi 1969 benknoti ya dola ya Marekani ilikuwa na ahadi ya kwamba serikali ya Marekani atampatia kila mtu dhahabu kulingana na thamani ya dola hizi akipenda kuibadilisha. Usawa huu na thamani ya dhahabu ulifutwa. Leo hii dola ya Marekani ni pesa ya kuiamini serikali kama pesa zote. Maana yake watumiaji husadiki ya kwamba serikali haitachapisha dola kushinda uwezo wa uchumi na thamani ya bidhaa zilizopo nchini.

Tangu mwisho wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia 1945 dola ya Marekani imekuwa pesa kuu duniani na sehemu kubwa ya biashara ya kimataifa hukadiriwa kwa bei za dola hizi. Lakini tangu kupatikana kwa Euro mwaka 1999 umuhimu wa dola ya Marekani imeanza kupungua polepole.