Periheli : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
No edit summary
No edit summary
Mstari 13: Mstari 13:


[[Category:Astronomia]]
[[Category:Astronomia]]
{{wikinyota}}

Pitio la 16:48, 24 Novemba 2018

1. Sayari kwenye afeli yake 2. Sayari kwenye periheli yake 3. Jua

Periheli (ing. perihelion) ni mahali katika obiti ya sayari au magimba mengine ya angani ambako ni karibu zaidi na jua. Jina linatokana na kigiriki Περι peri (karibu) na Ήλιο "helio" (jua).

Kinyume chake ni afeli inayomaanisha sehemu ya obiti iliyo mbali kabisa na jua. Obiti ni jina la njia ya gimba kuzunguka jua.

Majina haya hutumiwa kwa sababu obiti huwa na umbo la duaradufu na kwenye mzingo wa duaradufu kuna sehemu za karibu na sehemu za mbali na kitovu. Yasingekuwa na maana kama obiti ingekuwa duara kamili kwa sababi kwenye mzingo wa duara kila nukta ina umbali sawa na kitovu. Lakini obiti zenye umbo la duara kamili hazitokei hali halisi.

Tazama pia

  • Perijio (sehemu ya karibu kwenye obiti ya kuzunguka dunia)
Mradi wa Astronomia Makala hii imewahi kukaguliwa na kuboreshwa kwenye warsha ya pamoja ya Jenga Wikipedia ya Kiswahili, Wikimedia Community User Group Tanzania na ASSAT. Imepewa hali ya ulinzi. Tunaomba mapendekezo yote ya usahihisho na nyongeza zipelekwe kwanza kwenye ukurasa wa majadiliano