MB Salone
MB Salone | |
---|---|
| |
Maelezo ya awali | |
Jina la kuzaliwa | Mohamed Bailor Barrie |
Asili yake | Sierra Leone, Africa |
Aina ya muziki | |
Kazi yake | Mtayarishaji wa rekodi, mwimbaji, Mhariri wa Blogu, Mpiga Picha |
Miaka ya kazi | 2011 – |
Studio | Medialegendz LLC |
Ame/Wameshirikiana na | Dj Unk Young Dro Lil Key Fred Marshall Mike Snotty Miller Mr. Wilson Zay Hilfiger Thisis50 |
Tovuti | https://www.mbsalone.com/ |
Mohamed Bailor Barrie (anajulikana zaidi kwa jina lake la kisanii kama MB Salone; alizaliwa Freetown, Sierra Leone, 17 Agosti 1990) ni mtayarishaji wa rekodi za muziki wa Hip hop, Trap na RNB, wa Los Angeles, Marekani mwenye asili ya nchi ya Sierra Leone, Afrika. [1] [2][3] MB Salone alianza utayarishaji rekodi mwaka wa 2011 akiwa mwanafunzi wake Mike Snotty Miller; mtayarishaji rekodi na mshindi wa tuzo za Grammy.[2][3] Salone ametayarisha rekodi mingi na rekodi zingine zake zilitumika katika vipindi za MTV kama vile muziki wake Lil Key - "Shorty Right There" aliourekodi akishirikiana naye Mr. Wilson. Rekodi hii ilitumika katika vipindi "My Super Sweet 16" na "Rap Game" msimu wa pili za MTV.[2][3] MB Salone ameteuliwa kama mtayarishaji bora wa mwaka kwa tuzo za wananchi wa Afrika Magharibi ("The West African Citizens Awards") za mwaka wa 2018.
Katika utenda kazi wake amewatayirishia wanamuziki wengi vibao ikiwemo Fred Marshall, Kylie Beniamino, DJ UNK, Tokyo Jetz, Yung Dro, Lil Key, T. Rone and wengine wengi. [1][4][5]
Binafsi
[hariri | hariri chanzo]MB Salone ametoka katika kabila la Wafulani wa Sierra Leone. Alizaliwa wakati nchi yake iliathirika na vita dhidi ya mali asili hasa almasi ya Sierra Leone. Akiwa mtoto mdogo wa miaka miwili alipata ajali mbaya alipoanguka chini kutoka gorofa la pili na kupasua paji lake la uso. Ilimulazimu kufanyiwa operesheni iliomuacha na kovu kubwa usoni anayoivalia mpaka wa leo.[3]
Akiwa miaka sita aliponea chupu chupu kutekwanyara na waasi wa kivita akiwa na dadake na muda mfupi baadaye alikimbilia Marekani kama mkimbizi asiye na kibali. Alikimbilia Jacksonville na kuungana na baadhi ya wanafamilia wake waliokuwa wamemtangulia. Alijiunga na shule za malekani kuendeleza masomo yake.[3]
Shuleni MB Salone alikuwa na wakati mgumu na hakuhitimu mitahani yake. Mara kwa mara alijipata taambani tokana na uchechi wake na utovu wa nidhamu uliochangia pakubwa kufeli mitihani.[5] Akiwa darasa la saba, unga ulizidi maji na akatiwa mbaroni alipoiba duka la Target Jacksonville, Florida.
Bado akiwa shuleni shauku yake ya muziki ilikuwa inakita mizizi na mwaka wa 2007 akiwa shule ya upili ya Wolfson mle Jacksonville, Florida alikuwa ashaanza kutengeneza biti za R&B and Trap. Kwa bahati mbaya uundaji wa muziki ulikuwa unachukua muda wake mwingi na masomo yake shuleni yaliendelea kudidimia na hatimaye alifukuzwa shuleni akiwa mwaka wake wa mwisho kwa kutohudhuia darasa mara mingi.
MB Salone alikaa alibahatika kurudi shuleni mwaka wa 2014 nakujiunga na chuo cha kiufundi cha wanajamii ya Prince Georges (Prince George's Community College) iliyoko Largo, katika kaunti ya Prince George's, Maryland . Alifuzu programu ya GED na akapata stashahada yake mwaka wa 2015.[3]
Utayarishaji Rekodi
[hariri | hariri chanzo]Maisha ya MB Salone katika muziki yalianza mwaka wa 2011 alipokutana naye Fred Marshall nje ya duka la dawa la Walreens Atlanta akiuza rekodi alizokuwa ameunda. Fred Marshall alifurahishwa na kazi yake na akachukua hatua ya kumjulishana naye Mike Snotty Miller, Sonny Digital na Dj UNK.[3]
Mike Snooty Miller alimchukua MB Salone kama mwanafunzi wake na kumfunza sanaa ya uundaji rekodi. MB Salone alishilikiana naye Mike Snotty katika kazi mingi ikiwemo rekodi "Carousel" yake Kylie Beniamino na kadhaa za Dj Unk. Pia alifanya kazi na wanamuziki wengine wengi ikiwemo Yung Dro, T. Rone, Tokyo Jetz na wengine wengi waliokuwa wachanga uimbaji.[1][3]
Mwaka wa 2017 MB Salone alipatiwa nafasi kufanya kazi naye Lil Key na akiwa naye Bwana Wilson waliunda kibao chake "Shorty Right There". Kibao hiki kilifanikiwa kutumika na MTV baadaye katika vipindi zake "My Super 16" na kipindi "Rap Game" msimu wa pili. MB Salone pia aliunda video ya rekodi hii akishirikiana naye DJ. J. Remy.[3]
Mbali na kuwasaidia wanamuziki wengine, MB Salone pia arishirikia naye T. Rone mwaka 2017 wakatoa wimbo "Main Lady" na February mwaka uliofuata wa 2018 alitoa albamu yake ya muziki wa ala (instrumentals) yenye traki kumi na sita.[4]
Diskografia
[hariri | hariri chanzo]Albamu za kujitegemea
[hariri | hariri chanzo]- 2018: “Da Plug”[6], albamu ya muziki wa ala (instrumentals) yake MB Salone aliyoitayarisha mwenyewe - Medialegendz LLC
Kazi Alizotayarisha
[hariri | hariri chanzo]- 2017: "Shorty Right There" – Lil Key (MB Salone alitayarisha rekodi akishirikia naye Bwana Wilson na video akishirikiana naye DJ J. Remy)
- 2018: "The World"[7] – City of Angelo akishirikiana naye Zay Hilfigerrr (iliyotalishwa na MB Salone) - Medialegendz LLC
Kazi Alizoshirikishwa
[hariri | hariri chanzo]- 2017: "Main Lady"[8] – MB Salone akishirikiana naye T. Rone (iliyotayarishwa na MB Salone) - Medialegendz LLC
Tuzo na Uteuzi
[hariri | hariri chanzo]Mwaka | Kazi iliyoteuliwa | Tuzo | Matokeo |
---|---|---|---|
2018 | MB Salone mwenyewe | Tuzo za Wananchi wa Africa Magharibi (The West African Citizen Awards) – mtayarishaji rekodi wa mwaka | ameteuliwa (tuzo bado kupeanwa) |
Kazi nyingine
[hariri | hariri chanzo]Mbali na kutayarisha rekodi MB Salone pia ni mhariri wa blogu. Yeye ni mmoja wa wahariri wakuu wa blogu " Thisis50" yake mwanamuziki 50 Cent [1][3]
MB Salone pia ni mpiga picha wateja wake wakiwemo watu mashuhuri kama vile Lawrence Robinson, Alton Williams, Mekhi Phifer, na pia mwamichezo Gabby Douglas.[1] . Yeye pia ni mmoja wapo wa wapiga picha wa kampuni ya nywele RPG Hair.[1][3][4]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ 1.0 1.1 1.2 1.3 1.4 1.5 "SIERRA LEONEAN MUSIC PRODUCER MB SALONE EXCELS IN THE US – Salone Today". Salone Today (kwa American English). 27 Februari 2018. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2018-07-18. Iliwekwa mnamo 2018-07-12.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ 2.0 2.1 2.2 Kanja, Peter. "MB Salone". IMDb (kwa American English). Iliwekwa mnamo 12 Julai 2018.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ 3.00 3.01 3.02 3.03 3.04 3.05 3.06 3.07 3.08 3.09 3.10 Peter K. (5 Machi 2018). "The Sad Dark Story Behind MB Salone Childhood". Kilele 254 (kwa American English). Iliwekwa mnamo 12 Julai 2018.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ 4.0 4.1 4.2 Salone Music (Machi 2018). "Top Sierra Leone Producer - MB Salone Releases His Anticipated Instrumental Album". ZambianMusic.net (kwa American English). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2018-07-18. Iliwekwa mnamo 12 Julai 2018.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ 5.0 5.1 Music in Africa. "MB Salone". Music In Africa Website (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 12 Julai 2018.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "MB Salone - Da Plug". Discogs (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2018-07-12.
- ↑ The World (feat. Zay Hilfigerrr) - Single by City Of Angelo (kwa Kiingereza (Canada)), 22 Juni 2018, iliwekwa mnamo 12 Julai 2018
{{citation}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "MB Salone, T. Rone - Main Lady". Discogs (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2018-07-12.
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- https://www.mbsalone.com/ Ilihifadhiwa 25 Agosti 2018 kwenye Wayback Machine.