Nenda kwa yaliyomo

Lola Akinmade Åkerström

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Lola Akinmade Akerstrom

Nchi Nigeria
Kazi yake mpiga picha na mwandishi

Lola Akinmade Åkerström ni mpiga picha na mwandishi wa safari kutokea Nigeria aliyeko Stockholm, Sweden.[1] Yeye ndiye mhariri mkuu wa Slow Travel Stockholm.[2]

Kazi zake zimeangaziwa katika National Geographic Traveller BBC, na CNN, miongoni mwa machapisho mengine.[3] Alisoma Mfumo wa habari ya Jiografia (GIS) katika Chuo kikuu cha Maryland. [4]

Maisha ya Awali na Elimu

[hariri | hariri chanzo]

Maisha yake ya awali yalianzia mjini Lagos, Kusini Magharibi mwa Nigeria, ambapo alimaliza elimu yake ya awali kabla ya kuhamia Marekani akiwa na umri wa miaka 15.[5] Alipokea digrii ya uzamili katika Mfumo wa Habari kutoka Chuo Kikuu cha Maryland.[6] Katika umri wa miaka 19, alipata usajili katika chuo kikuu cha Oxford huko Uingereza lakini alishindwa kuendelea kutokana na hali ya uchumi. Mnamo 2006, Åkerström alihamia Uswidi pamoja na Mumewe.[5]

Åkerström alianza kazi yake kama mwandishi wa habari kwa vitendo huko Eco-Challenge.[7]Alifanya kazi kwa miaka 12 kama msanidi programu wa GIS kabla ya kuwa mpiga picha mtaalamu. Kati ya 2006 na 2007, alijiunga na Mtandao wa Matador na kufanya kazi kama mhariri.[4] Mnamo Oktoba 2009 alijiuzulu uteuzi wake katika ulimwengu wa GIS kufuata mapenzi yake.[4] Mnamo Juni 2011, Åkerström alishiriki katika mpango wa kabla ya uteuzi ulioandaliwa na Quark Expeditions kumchagua mwandishi ambaye atasafiri kwenda Ncha ya Kaskazini kwa mradi wa kuandikisha mfumo-ikolojia wake.[8]Mnamo mwaka wa 2012 alishiriki katika mbio za kusafiri huko Fiji, ambapo alianza mchanganyiko wa ujuzi wake wa kusafiri, upigaji picha na uandishi[9]Mnamo mwaka wa 2016, alienda Italia kuhudhuria Urithi wa Dunia na Maeneo ya Urithi wa Dunia wa Unesco ya Sabbioneta na Mantua kwa uchunguzi. .[1]

  1. 1.0 1.1 Bastock, Louise. "Meet a traveller: Lola Akinmade Åkerström, travel writer and photographer", Lonely Planet, 2016-05-06. (en) 
  2. "Contributors", Slow Travel Stockholm. Retrieved on 2021-03-27. (en-US) Archived from the original on 2018-09-26. 
  3. "Stop! This is what lagom truly means", 2017-06-30. (en) 
  4. 4.0 4.1 4.2 Awomodu, Gbenga. "Proudly African, In Love With Scandinavia & Exploring the World: Time Out with Lola Akinmade, Award-Winning Travel Writer & Photographer". BellaNaija (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2018-09-26.
  5. 5.0 5.1 "Lola Akinmade Åkerström: The GeoTraveler Who Finally Found Her Niche". Career. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2021-04-12. Iliwekwa mnamo 6 Juni 2016.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  6. "Lola Akinmade Akerstrom". The Advice Project. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2018-09-26. Iliwekwa mnamo 5 Mei 2016.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  7. Nellie Huang. "travel writing corner interview lola akinmade". wildjunk. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2016-08-16. Iliwekwa mnamo 5 Mei 2016.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  8. staff. "Join Lola Akinmade to explore the North Pole". Nigeria Abroad magazine. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2016-08-06. Iliwekwa mnamo 5 Mei 2016.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  9. "interview Lola Akinmade Akestrom". jetting around. Iliwekwa mnamo 5 Mei 2016.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Lola Akinmade Åkerström kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.