Liz Mills

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Liz Mills ni kocha wa mpira wa kikapu kutoka Australia ambaye aliwahi kuwa kocha mkuu wa timu ya mpira wa kikapu ya wanaume ya nchini Moroko AS Salé. Yeye ndiye mkufunzi mkuu wa kwanza wa kike wa mpira wa kikapu kuongoza timu ya wanaume kwenye ubingwa wa bara FIBA, na pia ni kocha mkuu wa kwanza wa kike katika Ligi ya Mpira wa Kikapu Afrika (BAL) baada ya kuangazia mnamo mwaka 2022.Pia ni mkufunzi mkuu wa kwanza wa kike wa timu ya vilabu vya wanaume nchini Moroko, na katika ulimwengu wa Kiarabu.

Mills alianza kazi yake ya ukocha huko Sydney, Australia, mnamo mwaka 2002 akifanya kazi na timu ya vijana na timu ya juu ya wanawake. Tangu mwaka 2011, Mills amekuwa kocha mkuu na kocha msaidizi barani Afrika na timu za vilabu ya wanaume wakubwa, timu za kitaifa za vyuo vikuu vya wanaume na timu za kitaifa za wanaume.

Mnamomwaka 2021 Mills alikuwa mkufunzi mkuu wa timu ya Taifa ya Mpira wa Kikapu ya Wanaume ya nchini Kenya, na kuwa mwanamke pekee duniani wakati huo alisimamia timu ya taifa ya wanaume sio tu katika mpira wa kikapu bali katika mchezo wowote.[1][2]

  1. https://www.usnews.com/news/sports/articles/2021-03-19/liz-mills-takes-big-step-for-female-basketball-coaches
  2. http://www.fiba.basketball/afrobasket/2021/qualifiers/news/liz-mills-trailblazing-for-more-female-coaches-in-mens-basketball