Liam Neeson
Liam Neeson | |
---|---|
![]() Neeson kwenye sherehe ya Deauville American Film Festival, mnamo 2012 |
|
Amezaliwa | William John Neeson Ballymena, County Antrim, Ireland ya Kaskazini, Uingereza |
Kazi yake | Mwigizaji |
Miaka ya kazi | 1973–hadi leo |
Ndoa | Natasha Richardson (1994-2009) (kifo chake) |
William John "Liam" Neeson (amezaliwa tar. 7 Juni 1952) ni mwigizaji wa filamu wa Kiireland, ambaye amebadilisha uraia na kuwa raia wa Marekani tangu 2009.[1] Anafahamika zaidi kwa kucheza kama Oskar Schindler kwenye filamu ya Schindler's List, Michael Collins kwenye filamu ya Michael Collins, Qui-Gon Jinn kwenye mfululizo wa filamu ya Star Wars Episode I: The Phantom Menace na Aslan kwenye mfululizo wa filamu za The Chronicles of Narnia.
Pia, amepata kucheza kwenye mafilamu mengine maarufu sana kama vile Darkman, Rob Roy, Kingdom of Heaven, Batman Begins na Taken. Amecheza wahusika kadhaa wanaohusiana na watu wa kweli. Wahusika hao ni pamoja na Oskar Schindler, Michael Collins na Alfred Kinsey.
Marejeo[hariri | hariri chanzo]
Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]
- ITV Local Interview at premiere of Taken
- Liam Neeson kwenye Internet Movie Database
- Liam Neeson katika Internet Broadway Database
- Liam Neeson at the British Film Institute's Screenonline
- The American Ireland Fund Performing Arts Award 2008
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
|
![]() |
Makala hii kuhusu mwigizaji filamu fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Liam Neeson kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |