Leptis Magna

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Geti ya Septimus Severus katika magofu ya Leptis Magna

Leptis Magna ilikuwa mji muhimu wa Dola la Roma katika jimbo la Afrika. Magofu yake yapo takriban kilomita 130 mashariki ya Tripoli (Libya).

Mji ulianzishwa na Wafinisia ikawa chini ya Karthago halafu ikaingizwa katika Dola la Roma. Ilikuwa kitovu muhimu ya biashara kati ya Sahara na Roma ikapanuka hadi kufikia wakazi 100,000.

Kaisari Septimius Severus aliyekuwa mwenyeji wa mji aliupamba kwa majengo mazuri na kuupa haki ya mji wa Italia iliyomaanisha ilisamehewa kodi.

Katika karne ya tatu mji ulirudi nyuma baada ya kushambuliwa mara kwa mara na makabila ya Sahara. Baada ya uvamizi wa Wavandali mwaka 455 halafu wa Waarabu mwaka 647 wakazi wote waliondoka.

Magofu yake yalihifadhiwa katika hali ya hewa yabisi hadi leo hii.