Lango:Ulaya/Makala iliyochaguliwa/1

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Hohenzollernbrücke Köln

Köln (pia: Kolon (kutokana na Kiing. Cologne; Kijerumani cha kienyeji: Kölle) ni mji wa Kijerumani kando la mto Rhine mwenye wakazi 970,000. Maana ya kiasili ya jina ni "koloni".

Köln ni mji mkubwa wa nne wa Ujerumani na mji mkubwa wa jimbo la Rhine Kaskazini-Westfalia (Nordrhein-Westfalen). Mji umejulikana nchini kwa aina yake ya pekee ya bia. Köln ni pia kitovu cha Waafrika katika Ujerumani. Pamoja na wanafunzi wengi kutoka Afrika kuna pia taasisi kama huduma ya Sauti ya Ujerumani (Deutsche Welle) zinazoajiri Waafrika wengi. Kuna hata vilabu ambako bia aina ya Tusker kutoka Kenya inauzwa.