Ziwa Nikaragua
Mandhari
(Elekezwa kutoka Lake Nicaragua)
| |
Nchi zinazopakana | Nikaragua |
Eneo la maji | km2 41,600 |
Kina cha chini | m 45 |
Mito inayoingia | Río Tipitapa |
Mito inayotoka | Mto San Juan |
Kimo cha uso wa maji juu ya UB |
m 31 |
Ziwa Nicaragua ndilo ziwa kubwa zaidi katika Amerika ya Kati. Liko kusini mwa Nikaragua, karibu na mpaka na Kosta Rika. Ziwa hilo linapokea sehemu ya maji yake kutoka Ziwa Managua kupitia mto mdogo wa Tipitapa.
Ndani ya Ziwa Nikaragua kuna visiwa vidogo zaidi ya 400, visiwa vikubwa vitatu na volkeno mbili.
Maji ya ziwa hutoka kupitia Mto San Juan ambao ni pia mpaka na Kosta Rika na kuelekea Bahari ya Karibi.
Makala hii kuhusu eneo fulani bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu eneo hilo kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Je, unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.
|