Nenda kwa yaliyomo

Rasi ya Labrador

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Labrador Peninsula)
Rasi ya Labrador
Misitu ya Labrador

Labrador ni rasi kubwa katika mashariki ya Kanada yenye eneo la kilomita za mraba 1,400,000. Inazungukwa na maji kwa panda tatu:

Upande wa kusini-magharibi Labrador imeunganishwa na Kanada bara.

Rasi hii ina wakazi wachache sana imefunikwa hasa na misitu na tundra. Kiutawala imegawiwa baina ya majimbo ya Quebec na Newfoundland na Labrador.

Wakazi asilia walikuwa Maindio na Waeskimo katika kaskazini ya Labrador. Mnamo mwaka 1,000 Waviking kutoka Norwei walifika waliochukua miti kwa vijiji vyao pale Greenland inayokosa misitu.

Jina la Labrador inatokana na mbaharia na mpelelezi Mreno aliyeitwa Lavrador aliyefika mnamo 1498 na kuchora ramani ya pwanzi zake. Alitangaza utawala wa kireno juu ya nchi hizi lakini hakuna Mreno aliyemfuata.

Tangu 1534 Wafaransa walianza kuunda vituo vyao katika Quebec kwenye kusini ya Labrador. Kwa muda mrefu walilenga hasa biashara na Maindio. Katika karne ya 17 walifuata polepole pia walowezi Wafaransa waliojenga vijiji na miji katika kusini karibu na mto Saint Lawrence.

Baada ya Vita ya Miaka Saba (1856-63) maeneo yote ya Ufaransa katika Kanada ya leo yalitwaliwa na Uingereza na hivyo pia Labrador iliingizwa chini ya utawala wa Kiingereza na hivyo kuwa sehemu ya Kanada ya kisasa.