Nenda kwa yaliyomo

L'Animal

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
L'Animal
L'Animal Cover
Studio album ya Khalid Kumbuka (KK)
Imetolewa 26 Julai, 2017
Imerekodiwa 2014-2016
Aina Hip hop
Wendo wa albamu za Khalid Kumbuka (KK)
L'Aniamal
(2017)
Single za kutoka katika albamu ya L'Animal
  1. "Defiant"
    Imetolewa: 2015
  2. "Ready to Go"
    Imetolewa: Julai, 2016

"L'Animal" ni jina la albamu ya kwanza kutoka kwa rapa Khalid Kumbuka (KK) wa Kwanza Unit Foundation. Albamu ilitolewa mnamo tarehe 26 Julai, 2017. Albamu imetayarishwa na watayarishaji mbalimbali ikiwa ni pamoja na Henry Muoria Jr, Ivan "Odie" Oduol, Othman "Palla" Palla, Rodgers "RAW" Charles, Luciano "Lucci" Tsere, Alfred "Throneboy" Rodgers na kufanyiwa uchangaji na uboreshwaji na Emmanuel Mtui. Albamu imeshirikisha wasanii mbalimbali wa hip hip Tanzania ikiwa ni pamoja na KBC, Zaiid, Brian Simba, Throneboy, Naomisia, Chi na Damian Soul.

Utayarishaji wa albamu imerekodiwa kwa kipindi kama cha miaka miwili na nusu; kuanzia Disemba 2014 hadi Mei 2016 (kwa kurekodiwa katika mastudio mbalimbali katika kipindi hiki chote). Mnamo Juni 2016, KK alisafiri nchini Uingereza kwa muda wa wiki 3 na akiwa huko alirekodi nyimbo 10, sita katika hizo zimeonekana katika albamu. Kuanzia Julai 2016, muda alikuwa akichagua nyimbo zipi zitafaa kwa ajili ya albamu - ambazo nyengine alirekodi tangu 2014 hadi hapo alipoanza kazi ya kuzifanyia uchanganyaji na kuziboresha, picha za promesheni na makasha yake na mipango mingine kwa ajili ya utoezi wa albamu. Albamu alitoa kwa kuonesha umma kama anatoka katika asili ya hip hop halisi ya Tanzania. Ukizingatia KK ni mdogo wa hayati Nigga One ambaye pia alikuwa miongoni mwa waanzilishi wa hip hop ya Tanzania na mmoja kati ya waliotoa wazo la awali la uanzishwaji wa Kwanza Unit. Adili au Nigga One alifariki na ajali ya gari mnamo mwaka wa 1993 jijini Dar es Salaam. Mnamo nwaka 2015 alitoa singo ya kwanza kutoka katika albamu Defiant na tarehe 24 Agosti alitoa Ready to Go aliyourekodi akiwa Uingereza na video kupigiwa hukohuko.

Historia ya albamu

[hariri | hariri chanzo]
Upande wa nyuma wa kasha la albamu ya L'Animal.

KK anaeleza kuwa madhumuni ya albamu hii kwanza ikiwa kazi ambayo ni binafsi kwake, tangu alivyoanza harakati hizi za rap. Suala la kutoa albamu lilikuwa moyoni yake ipo siku atatoa albamu ambayo itaelezea maisha yake, njia alizopitia kwenye tasnia hadi sasa, vikwazo na changamoto za maisha alizopita na kadhalika. Nia hasa ilikuwa kuionesha jamii iliyomzunguka kuwa inawezekana kupambana na hali yako bila kukata tamaa.

Pili alitaka kuhamasisha wasanii wachanga kutokata tamaa kwani kama una nia njia itaonekana tu na wala hakuna haja ya kujishtukia na kadhalika - huku akisisitiza subira ndiyo msingi wa mafanikio kwani nae pia ilimchukua muda mrefu hadi kufikia malengo yake. Tatu alitaka kuwakilisha Kwanza Unit na Nigga One kwani anadhani tasnia imesahau mchango wao, jambo ambalo aliona kama aibu vile; pia alitaka kuingiza midundo mipya katika tasnia ya muziki wa hip hop ya Tanzania. Vilevile alitaka kuona ma-DJ na wasanii wenzake watambue umuhimu wa wao kukua kimziki na kutengeneza mabadiliko ya midundo ya Tanzania iendane na soko la dunia na bara la Afrika kwa ujumla.

Orodha ya nyimbo

[hariri | hariri chanzo]

Hii ni orodha ya nyimbo zinazopatikana katika albamu hii na maelezo ya watayarishaji wake.

Na.Jina la wimboMtunziMtayarishajiMaelezo
1Survival Is BasicK. KumbukaIvan “Odie” OduolImechanganywa na kuwekwa sawa na: Emmanuel Mtui katika studio za Tipa Tone Soundworks.

Imerekodiwa: Throne Tower Records, Dar es Salaam Imerekodiwa na: Alfred “Throneboy’ Rodgers

2DefiantK. Kumbuka na A. Mnete)Othman "Palla" PallaImechanganywa na kuwekwa sawa na: Emmanuel Mtui katika studio za Tipa Tone Soundworks

Imerekodiwa: Tattoo Studios, Dar es Salaam Sauti za ziada: Abdullah Jamal Mnete

3For The CityK. Kumbuka na H. MuoriaHenry Muoria JrImechanganywa na kuwekwa sawa na: Emmanuel Mtui katika studio za Tipa Tone Soundworks

Imerekodiwa: UKOverstood Studios, London

4The ManK. KumbukaRodgers "RAW" Charles KiegezoImechanganywa na kuwekwa sawa na: Emmanuel Mtui katika studio ya Tipa Tone Soundworks

Imerekodiwa: FishCrab Records, Dar es Salaam

5300K. Kumbuka, B. Simba, A.RodgersAlfred "Throneboy" RodgersWimbo huu kamshirikisha: Simba na Throneboy

Imechanganywa na kuwekwa sawa na: Emmanuel Mtui katika studio ya Tipa Tone Soundworks Imerekodiwa: Throne Tower Records, Dar es Salaam Sauti za ziada: Brian Simba na Alfred Rodgers

6Ready To GoK. Kumbuka na H. MuoriaHenry Muoria JrImechanganywa na kuwekwa sawa na: Emmanuel Mtui katika studio ya Tipa Tone Soundworks

Imerekodiwa: UKOverstood Studios, London

7Ice BabyK. Kumbuka na H. MuoriaHenry Muoria JrImechanganywa na kuwekwa sawa na: Emmanuel Mtui katika studio ya Tipa Tone Soundworks

Imerekodiwa: UKOverstood Studios, London

8You Can Get ItK. Kumbuka na H. MuoriaHenry Muoria Jr na Emmanuel MtuiImechanganywa na kuwekwa sawa na: Emmanuel Mtui katika studio ya Tipa Tone Soundworks

Imerekodiwa: UKOverstood Studios, London na Beem Studios, Dar es Salaam Sauti za ziada: Naomisia Mchaki

9WawiliK. Kumbuka na H. MuoriaHenry Muoria Jr na Alfred "Throneboy" RodgersImechanganywa na kuwekwa sawa na: Emmanuel Mtui katika studio ya Tipa Tone Soundworks

Imerekodiwa: UKOverstood Studios, London na Beem Studios, Dar es Salaam Sauti za ziada: Naomisia Mchaki

10Doing It WellK. KumbukaHenry Muoria JrImechanganywa na kuwekwa sawa na: Emmanuel Mtui katika studio ya Tipa Tone Soundworks

Imerekodiwa: UKOverstood Studios, London

11BreatheK. KumbukaHenry Muoria JrImechanganywa na kuwekwa sawa na: Emmanuel Mtui katika studio ya Tipa Tone Soundworks

Imerekodiwa: UKOverstood Studios, London

12MargaretK. Kumbuka na A. TemuLuciano "Lucci" Tsere, Alfred "Throneboy" RodgersImechanganywa na kuwekwa sawa na: Emmanuel Mtui katika studio za Tipa Tone Soundworks

Imerekodiwa: TransforMax Records, Dar es Salaam, Throne Tower Records, Dar es Salaam na Beem Media Ltd, Dar es Salaam

13MbaliK. Kumbuka, Kibacha Singo, D. MihayoOthman "Palla" PallaImechanganywa na: Emmanuel Mtui katika studio za Tipa Tone Soundworks

Imerekodiwa: Nakiete Studios, Dar es Salaam Sauti za ziada: Damian Mihayo

Viungo vya Nje

[hariri | hariri chanzo]