Nenda kwa yaliyomo

Kutokwa na damu kwa uterasi kusiko kwa kawaida

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Kutokwa na damu kwa uterasi kusiko kwa kawaida
Mwainisho na taarifa za nje
Kundi MaalumuMagonjwa ya wanawake
DaliliKiasi kisicho cha kawaida, kwa njia ya mara kwa mara isiyo ya kawaida, kwa muda mrefu, au kutokwa damu kwa uterasi kwa kiasi kingi sana[1]
VisababishiMatatizo ya uzalishaji wa yai la kike, nyuzinyuzi za tumboni, utando wa uterasi kukua hadi kwenye ukuta wa uterasi, vipolipu vya uterasi (polyps), matatizo ya msingi ya kutokwa na damu, madhara yatokanayo na udhibiti wa uzazi , saratani[2]
Njia ya kuitambua hali hiiKulingana na dalili, kazi ya damu, picha za matibabu, hysteroscopy[3]
Utambuzi tofautiMimba ya nje ya kizazi[4]
MatibabuUdhibiti wa uzazi kwa homoni, madawa ya kuongeza homoni ya kuachia gonadotropini, asidi ya tranexamic, NSAIDs, upasuaji[1][5]
Idadi ya utokeaji wakeKawaida kwa kiasi fulani[3]

Kutokwa na damu kwa uterasi kusiko kwa kawaida (AUB), pia inajulikana kama kutokwa na damu kwa uke kusiko kwa kawaida, ni kutokwa na damu kwa uke kutoka kwenye uterasi kwa njia ambayo mara kwa mara kwa njia isiyo ya kawaida na kwa muda mrefu kupita kiasi, nayo huwa nzito kuliko kawaida, au kwa njia isiyo ya kawaida.[1][2] Neno kutokwa na damu kwa uterasi isiyofanya kazi ipasavyo lilitumika wakati hakuna sababu ya msingi ya hilo.[2] Kutokwa na damu ukeni baada ya kukoma hedhi sio kawaida.[6] Kutokwa na damu kwa uke wakati wa ujauzito hutengwa kando na hali hii.[2] Upungufu wa damu (anemia) kutokana na ukosefu wa madini ya chuma inaweza kutokea na ubora wa maisha unaweza kuathiriwa vibaya.[7]

Sababu zake kuu zinaweza kujumuisha matatizo ya udondoshwaji wa yai, nyuzinyuzi, utando wa uterasi kukua hadi kwenye ukuta wa uterasi, vipolipu vya uterasi (polyps), matatizo ya msingi ya kutokwa na damu, madhara yatokanayo na udhibiti wa uzazi au saratani.[2] Zaidi ya kategoria moja ya sababu inaweza kutumika katika kesi ya mtu binafsi.[2] Hatua ya kwanza ya urekebishaji ni kuondoa uvimbe au ujauzito.[2][5] Picha za uchunguzi wa kimatibabu au hysteroscopy inaweza kusaidia katika utambuzi.[3]

Matibabu yake yanategemea sababu ya msingi.[3][2] Chaguo zinaweza kujumuisha udhibiti wa homoni ya uzazi, madawa ya kuongeza uzalishaji wa homoni ya kuachia gonadotropini ( GnRH), asidi ya tranexamic, NSAIDs na upasuaji kama vile uondoaji wa endometriamu au hysterectomy.[1][5] Kutokwa na damu kwa uterasi kusiko kwa kawaida huathiri takriban 20% ya wanawake wenye umri wa uzazi.[3]

  1. 1.0 1.1 1.2 1.3 "Abnormal Uterine Bleeding". ACOG. Machi 2017. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 11 Septemba 2018. Iliwekwa mnamo 11 Septemba 2018.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. 2.0 2.1 2.2 2.3 2.4 2.5 2.6 2.7 Bacon, JL (Juni 2017). "Abnormal Uterine Bleeding: Current Classification and Clinical Management". Obstetrics and Gynecology Clinics of North America. 44 (2): 179–193. doi:10.1016/j.ogc.2017.02.012. PMID 28499529.{{cite journal}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. 3.0 3.1 3.2 3.3 3.4 Whitaker L, Critchley HO (Julai 2016). "Abnormal uterine bleeding". Best Pract Res Clin Obstet Gynaecol. 34: 54–65. doi:10.1016/j.bpobgyn.2015.11.012. PMC 4970656. PMID 26803558.{{cite journal}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  4. "Vaginal Bleeding". Merck Manuals Professional Edition. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 14 Julai 2019. Iliwekwa mnamo 11 Septemba 2018.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  5. 5.0 5.1 5.2 Cheong, Y; Cameron, IT; Critchley, HOD (1 Septemba 2017). "Abnormal uterine bleeding". British Medical Bulletin. 123 (1): 103–114. doi:10.1093/bmb/ldx027. PMID 28910998.{{cite journal}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  6. Sung, Sharon; Abramovitz, Aaron (2023). "Postmenopausal Bleeding". StatPearls. StatPearls Publishing. PMID 32965859. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2023-03-24. Iliwekwa mnamo 2023-10-30.
  7. Kovalenko, Mariya; Velji, Zain Azim; Cheema, Jaspreet; Datta, Shreelata (1 Novemba 2021). "Intermenstrual and postcoital bleeding". Obstetrics, Gynaecology & Reproductive Medicine. 31 (11): 310–316. doi:10.1016/j.ogrm.2021.09.003. ISSN 1751-7214.{{cite journal}}: CS1 maint: date auto-translated (link)