Nenda kwa yaliyomo

Kukoma hedhi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Kukoma hedhi
Mwainisho na taarifa za nje
Kundi MaalumuMagonjwa ya wanawake
DaliliKukoma kwa hedhi kwa kipindi cha mwaka[1]
Miaka ya kawaida inapoanzaUmri wa miaka 49 hadi 52[2]
VisababishiKwa kawaida ni mabadiliko ya asili, upasuaji unaoondoa ovari, baadhi ya aina za Tiba za kemotherapi[3][4]
MatibabuHakuna, mabadiliko ya mtindo wa maisha[5]
DawaTiba ya homoni ya kukoma kwa hedhi, Klonidini, (clonidine), gabapentini, vizuizi maalumu vya utumiaji tena wa serotonini[5][6]

Kukoma hedhi (Menopause), pia inajulikana kama climacteric, ni wakati katika maisha ya wanawake wengi ambapo hedhi hukoma kutoka kabisa, na hawawezi tena kuzaa watoto. Kukoma hedhi kwa kawaida hutokea kati ya umri wa miaka 49 na 52.[2] Wataalamu wa kimatibabu mara nyingi hufafanua kukoma kwa hedhi kuwa kumetokea wakati mwanamke hajavuja damu ya hedhi kwa mwaka mmoja. Hali hii inaweza pia kufafanuliwa kwa kupungua kwa uzalishaji wa homoni katika ovari.[7] Kwa wale ambao wamefanyiwa upasuaji wa kuondoa uterasi lakini bado wana ovari, kukoma hedhi kunaweza kuzingatiwa kuwa kulitokea wakati wa upasuaji au wakati viwango vyao vya homoni vilipungua.[7] Kufuatia kuondolewa kwa uterasi, dalili za kawaida huonekana mapema, kwa wastani wa miaka 45.[8]

Katika miaka kabla ya kukoma hedhi, hedhi ya mwanamke kwa kawaida hutokea kwa mpangilio usio wa kawaida,[9] ambayo ina maana kwamba hedhi inaweza kuwa ya muda mrefu au mfupi au kuwa nyepesi au nzito zaidi katika kiasi cha mtiririko.[9] Wakati huu, wanawake mara nyingi hupata hisia za ghafla za joto kali. Hili kwa kawaida hudumu kati ya sekunde 30 hadi dakika kumi, na linaweza kuambatana na kutetemeka, kutokwa na jasho na ngozi kuwa nyekundu.[9] Mara nyingi hisia za ghafla za joto kali huacha kutokea baada ya mwaka mmoja au miwili. Dalili zingine zinaweza kujumuisha ukavu wa uke, kutatizika kulala na mabadiliko ya hisia. Ukali wa dalili hutofautiana kati ya wanawake.[10] Ingawa kukoma kwa hedhi mara nyingi hufikiriwa kuwa kunahusiana na ongezeko la ugonjwa wa moyo, hili hasa hutokea kutokana na kuongezeka kwa umri na halina uhusiano wa moja kwa moja na kukoma kwa hedhi.[10] Katika baadhi ya wanawake, matatizo yaliyokuwapo kama vile hali ya ukuaji wa tishu za uterasi nje ya uterasi (Endometriosisi) au maumivu wakati wa hedhi yanaboreka baada ya kukoma kwa hedhi.[10]

Kukoma hedhi kwa kawaida ni badiliko la asili, kwani ovari hupungua polepole kwa ukubwa kadri umri unavyosonga.[11] Hili linaweza kutokea mapema kwa wale wanaovuta tumbaku.[12] Sababu nyingine ni pamoja na upasuaji wa kuondoa ovari zote mbili au aina fulani za tiba ya kemotherapi.[3] Katika kiwango cha kisaikolojia, kukoma kwa hedhi hutokea kwa sababu ya kupungua kwa uzalishaji wa homoni za estrojeni na projesteroni na ovari. Ingawa kwa kawaida haihitajiki, utambuzi wa kukoma hedhi unaweza kuthibitishwa kwa kupima viwango vya homoni katika damu au mkojo. Kukoma kwa hedhi ni kinyume cha kupata hedhi (menarche), wakati ambapo hedhi ya msichana huanza.[13]

Kwa kawaida, hali hii haihitaji matibabu mahususi.[5] Dalili zingine, hata hivyo, zinaweza kuboreshwa kwa matibabu.[5] Kuhusiana na hisia za ghafla za joto kali, mara nyingi inapendekezwa kuepuka kuvuta sigara, kutumia kafeini na pomb.[5] Kulala katika chumba baridi na kutumia feni kunaweza kusaidia.[5] Dawa zifuatazo zinaweza kusaidia: tiba ya homoni za kukoma hedhi (MHT), klonidini, gabapentini au vizuizi maalum vya uchukuaji tena wa serotonini.[5][6] Mazoezi yanaweza kusaidia kusuluhisha tatizo la kulala. [5] Ingawa MHT ziliagizwa mara kwa mara, kwa sasa zinapendekezwa tu kwa wale walio na dalili kali, kwa kuwa kuna wasiwasi kuhusu madhara yake. Ushahidi wa kiwango cha juu wa ufanisi wa dawa mbadala haujapatikana. Kuna ushahidi wa awali kuhusu ufanisi wa matumizi ya fytoestrojeni (phytoestrogens).[14]


Marejeleo

[hariri | hariri chanzo]
  1. Hitilafu ya kutaja: Invalid <ref> tag; no text was provided for refs named NIH2013Def
  2. 2.0 2.1 Takahashi TA, Johnson KM (Mei 2015). "Menopause". The Medical Clinics of North America. 99 (3): 521–34. doi:10.1016/j.mcna.2015.01.006. PMID 25841598.{{cite journal}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. 3.0 3.1 Hitilafu ya kutaja: Invalid <ref> tag; no text was provided for refs named NIH2013Con
  4. Hitilafu ya kutaja: Invalid <ref> tag; no text was provided for refs named NIH2013Ca
  5. 5.0 5.1 5.2 5.3 5.4 5.5 5.6 5.7 Hitilafu ya kutaja: Invalid <ref> tag; no text was provided for refs named NIH2013Tx
  6. 6.0 6.1 Krause MS, Nakajima ST (Machi 2015). "Hormonal and nonhormonal treatment of vasomotor symptoms". Obstetrics and Gynecology Clinics of North America. 42 (1): 163–79. doi:10.1016/j.ogc.2014.09.008. PMID 25681847.{{cite journal}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  7. 7.0 7.1 Sievert, Lynnette Leidy (2006). Menopause : a biocultural perspective (tol. la [Online-Ausg.]). New Brunswick, N.J.: Rutgers University Press. uk. 81. ISBN 9780813538563. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 10 Septemba 2017.
  8. International position paper on women's health and menopause : a comprehensive approach. DIANE Publishing. 2002. uk. 36. ISBN 9781428905214. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 10 Septemba 2017.
  9. 9.0 9.1 9.2 Hitilafu ya kutaja: Invalid <ref> tag; no text was provided for refs named NIH2013Sym
  10. 10.0 10.1 10.2 Hitilafu ya kutaja: Invalid <ref> tag; no text was provided for refs named PubMed2013
  11. Suster, David; Liu, Martina Z.; Lin, Douglas I. (2019). "3. Benign diseases of the ovary". Katika Zheng, Wenxin; Fadare, Oluwole; Quick, Charles Matthew; Shen, Danhua; Guo, Donghui (whr.). Gynecologic and Obstetric Pathology (kwa Kiingereza). Juz. la 2. Springer: Springer. uk. 96. ISBN 978-981-13-3018-6. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2 Agosti 2022. Iliwekwa mnamo 30 Julai 2022.{{cite book}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  12. Warren, volume editors, Claudio N. Soares, Michelle (2009). The menopausal transition : interface between gynecology and psychiatry (tol. la [Online-Ausg.]). Basel: Karger. uk. 73. ISBN 978-3805591010. {{cite book}}: |first= has generic name (help)CS1 maint: multiple names: authors list (link)
  13. Wood, James. "9". Dynamics of Human Reproduction: Biology, Biometry, Demography. Transaction Publishers. uk. 401. ISBN 9780202365701. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 10 Septemba 2017.
  14. Franco OH, Chowdhury R, Troup J, Voortman T, Kunutsor S, Kavousi M, Oliver-Williams C, Muka T (Juni 2016). "Use of Plant-Based Therapies and Menopausal Symptoms: A Systematic Review and Meta-analysis". JAMA. 315 (23): 2554–63. doi:10.1001/jama.2016.8012. PMID 27327802.{{cite journal}}: CS1 maint: date auto-translated (link)

[[Category:Magonjwa]]