Nenda kwa yaliyomo

Kungumanga

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Tunda la mkungumanga na jozi lake katikati ni kungumanga yenyewe.
Majani, maua na matunda ya kungumanga.

Kungumanga (kwa Kiingereza: nutmeg) ni mbegu ya miti ya aina mkungumanga (myristica fragrans). Asili ya miti hiyo iko kwenye visiwa vya Indonesia lakini leo ipo pia katika sehemu nyingine za tropiki pamoja na Afrika.

Mti huzaa matunda yenye urefu wa sentimita 8-10 na kipenyo cha sentimita 4-5. Ndani yake mna mbegu kama jozi ambayo ndiyo kungumanga yenyewe.

Mbegu na pia sehemu ya tunda inayofunika mbegu (rungu) hutumiwa na watu hasa kama kiungo cha chakula.

Inasemekana pia ya kwamba watu walijaribu kuitumia kama dawa ya ulevi lakini inakuja pamoja na athari zisizopendeza, kwa hiyo haikusambaa. Ikitumiwa mno inaweza kuleta matatizo ya kusumishwa.

Makala hii kuhusu mambo ya biolojia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kungumanga kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.