Kuki

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Kuki ni tafsiri ya muda ya neno la Kiingereza cookie.

Maana yake asili ni biskuti au keki ndogo, lakini neno la kuki linatumika ili kompyuta yenye kurasa za tovuti iweze kuwasaliana na watazamaji. Programu za tovuti hizi inahifadhi habari kadhaa za mtazamaji au mtumiaji (k.m. jina la mtumiaji, neno la siri, ruhusa, mapendekezo) kwenye kompyuta ya mtazamaji mwenyewe. Hivi mtazamaji anatambuliwa kila wakati anaingia kwenye tovuti hii.

Pendekezo la "kuki" limepelekwa mbele na Mradi wa Kilinux (Linux na Open Office kwa Kiswahili) wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Mradi wa kampuni ya Microsoft ya kuswahilisha programu ya "Windows" umependekeza kutumia neno "kidakuzi" pamoja na "kuki".

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]

Orodha ya maneno ya tarakishi ya mradi wa Kilinux kwenye Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Archived 15 Machi 2007 at the Wayback Machine.