Nenda kwa yaliyomo

Kokoro (chakula)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Kokoro(kitafunwa))

Kokoro ni kitafunwa maarufu nchini Nigeria. Kinaandaliwa na mchanganyiko wa unga wa mahindi, sukari, na muhogo au magimbi kisha kukaanga.[1] Kinauzwa sana maeneo ya Ogun, Nigeria.

Katika utafiti wa mwaka 1991 kuhusu vyakula vinavyouzwa kwa wanafunzi wa Lagos, chakula cha kokoro kilichukuliwa ili kufanyiwa utafiti zaidi kwa kibiolojia. Chakula hicho kilikutwa na bakteria wa aina kumi tofauti, ikiwemo bakteria wa sumu na kuharisha; hii ilipelekea kutolewa agizo la uandaaji wa vyakula hivyo kuzingatia zaidi afya ya mlaji kwa viandaliwe katika mazingira yaliyo salama.[2]

Katika utafiti wa kuongeza lishe, ilibainika kuwa soya iliyoondolewa mafuta au karanga huweza kutumika, lakini ladha na muonekano haukukubaliwa na takribani asilimia 10 ya unga.[3] Kitafunwa kingine cha kuongeza viritubisho kutoka kwenye kitafunwa cha kokoro ni mchanganyiko wa mahindi, soya na viungo kamahoho, vitunguu, chumvi, mafuta ya mnyonyo, na ndizi.[4]

  1. "Snacks: Kokoro II"
  2. https://archive.today/20130415134437/http://tropej.oxfordjournals.org/cgi/pdf_extract/37/5/266-a
  3. https://archive.today/20130415153722/http://pdfcast.org/cache/effect-of-partially-defatted-soybeans-or-groundnut-cake-flours-on-proximate-and-sensory-characteristics-of-kokoro
  4. Olusola Omueti; I. D. Morton. "Development by extrusion of soyabari snack sticks: a nutritionally improved soya—maize product based on the Nigerian snack (kokoro)". International Journal of Food Sciences and Nutrition,