Kobelo Chapombe

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Kobelo Chapombe
Amezaliwa Emilian Timon Kobelo
(1987-11-23)Novemba 23, 1987 Mwananyamala, Dar es Salaam, Tanzania
Dar es Salaam
Jina lingine Kobelo
Kazi yake Mwigizaji, mtunzi wa hadithi, mwongozaji, mhariri wa taswira mjongeo na mpiga picha
Miaka ya kazi 2002
Watoto 2

Emilian Timon Kobelo (amezaliwa Mwananyamala, Dar es Salaam, 23 Novemba 1987) ni mwigizaji, mtunzi wa hadithi, mwongozaji, mhariri wa filamu na mpiga picha kutoka nchini Tanzania. Anafahamika zaidi kwa uhusika wake wa Kobelo Chapombe ambao hucheza kama mraibu wa pombe.[1]

Maisha na kazi[hariri | hariri chanzo]

Emilian Timon Kobelo ni mtoto wa kwanza kuzaliwa katika famila ya watoto wanne waliozaliwa kati ya Timon Emilian Edward na Christina Stanford Senyagwa. Mwaka wa 2002 alijiunga na kikundi cha sanaa kilichoitwa 'Upendo Art Group.' Alitumikia sanaa yao kwa takribani miaka minne.

Mwaka wa 2006, alitoka kundini kisha akajiunga na Baba Watoto Youth Center. Mwaka wa 2008, alishiriki filamu mbili ambazo ziliandaliwa na kundi hilo.

Ilipotimu mwaka 2010, Kobelo na Bakari Salumu walifanya filamu mbili , Giza la Moyo - iliandikwa na Bakari Salumu. 2011 walirudi tena na kazi yao iliyoitwa Wizard of Heart iliandikwa na Kobelo. Kazi hiyo ilisambazwa na Steps Entertainment.

Mwaka wa 2014, alijiunga na kampuni ya Macho Media iliyokuwa chini ya Musa Yusuph Mahenge (Kitale). Akiwa hapa, alipata kushiriki katika filamu ya Shobo Dundo, Nikabu, Kimbiji, Mkubwa Bure, COSOTA, Kigugumizi, Kibena, Stanbakora na Akili.

2017 alishiriki kwenye tamthilia ya Maneno ya Kuambiwa iliyodumu miaka mitatu kupitia kituo cha runinga cha kulipia cha TVE. 2020 ameshiriki kaktika tamthilia ya "Binadamu Wabaya" iliyorushwa hewani kupitia TVE na idhaa ya YouTube maarufu kama IPOTV.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]