Nenda kwa yaliyomo

Kiwewe cha kichwa kutokana na unyanyasaji

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Kiwewe cha kichwa kutokana na unyanyasaji
Mwainisho na taarifa za nje
Kundi MaalumuPediatrics Edit this on Wikidata
DaliliInaweza kubadilika[1]
Muda wa kawaida wa kuanza kwakeChini ya miaka mitano[2]
VisababishiJeraha lisilo wazi, mtikisiko wa nguvu[1]
Njia ya kuitambua hali hiiUchunguzi wa CT[1]
KingaKuelimisha wazazi wapya[1]
Utabiri wa kutokea kwakeShida za kiafya za muda mrefu za kawaida[2]
Idadi ya utokeaji wakeWatoto watatu kwa kila watoto 10,000 kwa mwaka (Marekani)[1]
VifoHatari ya kifo ya ≈25% [2]

Kiwewe cha kichwa kutokana na unyanyasaji (kwa Kiingereza: Abusive head trauma, kifupi: AHT: linajulikana pia kama ugonjwa wa mtoto aliyetikiswa, kifupi: SBS) ni kiwewe cha kichwa cha mtoto kinachosababishwa na mtu mwingine (kama vile mlezi).[1] Dalili zake zinaweza kuwa ya siri hadi kuwa dhahiri[1], na zinaweza kujumuisha kutapika au mtoto kutotulia.[1] Mara nyingi hakuna dalili zinazoonekana za jeraha hili.[1] Matatizo ni pamoja na kifafa, kuharibika kwa uwezo wa kuona, kupooza kwa ubongo na kuharibika kwa utambuzi.[3][1]

Sababu yake inaweza kuwa kiwewe kisicho wazi au kutikisika kwa nguvu.[1] Mara nyingi hili hutokana na mlezi kuchukia mtoto kulialia.[2] Utambuzi wake unaweza kuwa mgumu kwani dalili zinaweza kuwa si maalumu.[1] Uchunguzi wa CT wa kichwa unapendekezwa ikiwa kuna wasiwasi.[1] Wakati kutokwa damu kwenye retina ni kawaida, inaweza pia kutokea katika hali nyinginezo.[1] Kiwewe hicho ni aina ya unyanyasaji wa watoto.[4]

Kuelimisha wazazi wapya inaonekana kuwa na manufaa katika kupunguza viwango vya hali hiyo.[1] Matibabu mara kwa mara huhitaji upasuaji, kama vile kuweka mrija wa kuondoa maji kwenye ubongo (cerebral shunt).[1] AHT inakadiriwa kutokea kwa watoto 3 hadi 4 kwa kila watoto 10,000 kwa mwaka.[1] Ugonjwa huu unatokea mara nyingi kwa wale walio chini ya miaka mitano.[2] Hatari ya kifo ni karibu 25%.[2] Utambuzi huo unaweza pia kuwa na matokeo ya kisheria kwa wazazi.[4]

  1. 1 2 3 4 5 6 7 8 9 10 11 12 13 14 15 16 17 Shaahinfar, A; Whitelaw, KD; Mansour, KM (Juni 2015). "Update on abusive head trauma". Current Opinion in Pediatrics. 27 (3): 308–14. doi:10.1097/mop.0000000000000207. PMID 25768258.{{cite journal}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. 1 2 3 4 5 6 "Preventing Abusive Head Trauma in Children". www.cdc.gov (kwa American English). 4 Aprili 2017. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 11 Juni 2017. Iliwekwa mnamo 9 Juni 2017.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. Advanced Pediatric Assessment, Second Edition (kwa Kiingereza) (tol. la 2). Springer Publishing Company. 2014. uk. 484. ISBN 9780826161765. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2017-11-05.
  4. 1 2 Christian, CW; Block, R (Mei 2009). "Abusive head trauma in infants and children". Pediatrics. 123 (5): 1409–11. doi:10.1542/peds.2009-0408. PMID 19403508.{{cite journal}}: CS1 maint: date auto-translated (link)