Kituo cha Umeme wa Maji cha Julius Nyerere
Mandhari
Kituo cha Umeme wa Maji cha Julius Nyerere (kwa Kiingereza: Julius Nyerere Hydropower Station (Stiegler's Gorge)) ni mradi mkubwa wa umeme wa maji unaojengwa kwenye mto Rufiji, Tanzania.
Mradi huo una uwezo wa kuzalisha megawati 2,115 za umeme, na kuongeza uzalishaji wa umeme nchini. Mradi huu unalenga kupunguza utegemezi wa umeme kutoka vyanzo vya nje, kuboresha huduma za umeme kwa wananchi na viwanda, na kuchangia katika maendeleo ya kiuchumi. Kituo hiki cha umeme na bwawa vinamilikiwa na unasimamiwa na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linalomilikiwa na serikali.
Ujenzi ulianza mnamo 2019 na unatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwaka 2024[1].
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Oirere, Shem (18 Agosti 2017). "Tanzania Revives 2,100-MW Hydro Power Project". Engineering News Record (ENR). Iliwekwa mnamo 3 Aprili 2018.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)
Makala hii kuhusu mambo ya uchumi bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Kituo cha Umeme wa Maji cha Julius Nyerere kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |