Kituo cha Anga

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Kituo cha Anga cha MIR, mnamo 1995

Kituo cha Anga (kwa Kiingereza: Space station) ni satelaiti inayozunguka Dunia kwenye obiti ya kudumu ikibuniwa kubeba wanaanga. Kusudi lake ni kuwezesha wanaanga kukaa kwenye anga-nje kwa kipindi fulani na kuendesha utafiti wa kisayansi wa aina mbalimbali. Kinaweza kutembelewa na vyombo vya anga-nje kama feri ya anga na kwa njia hiyo wanaanga wanaweza kufika au kurudi duniani na kupokea vifaa, fueli na chakula.

Tangu mwaka 2000 kuna Kituo cha Anga cha Kimataifa. Kilitanguliwa na vituo mbalimbali kama vile MIR (Urusi), Skylab (Marekani) na Tiagong (China).

Shabaha ya vituo vya anga ni kuchunguza athira ya hali pasipo graviti kwa mwili na nafsi ya binadamu na kutumia maabara zake kwa majaribio ya kisayansi[1]. Wanaanga hukaa kwa wiki au miezi kadhaa. Mwanaanga aliyekaa kwenye kituo cha anga kwa muda mrefu zaidi alikuwa Valeriy Polyakov (siku 437 kwenye MIR)[2]. [3].

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Space Stations. Oracle Thinkquest. Jalada kutoka ya awali juu ya 2014-02-24. Iliwekwa mnamo 20 February 2012.
  2. A History of Manned Space Missions. National Earth Science Teachers Association. Iliwekwa mnamo 4 May 2012.
  3. A history of space stations. Cable News Network (23 November 1998). Jalada kutoka ya awali juu ya 2013-01-19. Iliwekwa mnamo 25 May 2012.