Nenda kwa yaliyomo

Kitai-Dam

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Kitai-Dam ni lugha ya Kitai-Kadai nchini Vietnam, Laos, Uchina na Uthai inayozungumzwa na Watai. Mwaka wa 2002 idadi ya wasemaji wa Kitai-Dam nchini Vietnam imehesabiwa kuwa watu 699,000. Pia kuna wasemaji 50,000 nchini Laos (1995), 20,000 nchini Uchina (1995) na 700 nchini Uthai (2004). Kufuatana na uainishaji wa lugha, Kitai-Dam iko katika kundi la Kitai ya Kusini-Magharibi.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kitai-Dam kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.