Kisumbwa
Kisumbwa ni lugha ya Kibantu nchini Tanzania inayozungumzwa na Wasumbwa. Mwaka wa 1987 idadi ya wasemaji wa Kisumbwa imehesabiwa kuwa watu 191,000. Kufuatana na uainishaji wa lugha za Kibantu wa Malcolm Guthrie Kisumbwa iko katika kundi la F20.
Hali ya lugha ya Kisumbwa
[hariri | hariri chanzo]Katika uainishaji wa lugha za Kibantu, Kisumbwa kiliwekwa kwenye kundi la F la lugha za Kibantu, na kupewa na F.23 na Guthrie (1948). Kinahusiana na Kinyamwezi, Kisukuma, Kinilamba, Kirimi na lugha nyingine za kundi F (Guthrie 1948; 1967-71, Nurse na Philippson 1980 na Masele 2001). Kwa mujibu wa ushahidi wa kimsamiati, Kisumbwa kinaelekea kuwa karibu zaidi kwa Kinyamwezi kuliko lugha nyingine katika kundi hilo (Nurse na Philippson 1980). Licha ya hilo, wasemaji wa Kisumbwa kwa kipindi kirefu wamekuwa na uhusiano na wasemaji wa Kisubi (Biharamulo), Kirongo na Kizinza (Biharamulo, Geita na Sengerema), Kiha (Biharamulo), licha ya uhusiano uliopo na wasemaji wa Kinyamwezi na Kisukuma.
Lugha yenyewe inasemwa katika wilaya za Bukombe na Kahama (Mkoa wa Shinyanga), Geita na Sengerema (Mkoa wa Mwanza), Biharamulo (Mkoa wa Kagera) na Urambo (Uyowa) – Mkoa wa Tabora. Kwa kuzingatia takwimu za hesabu ya watu iliyofanyika mwaka 2002, idadi ya wasemaji wa Kisumbwa wanaweza kukadiriwa kama ifuatavyo: Bukombe: 137,115; Kahama: 100,377; Geita: 79,490; Biharamulo: 4,306; Ilemela: 85; Kishapu: 110; Kwimba: 152; Misungwi: 103; Nzega: 358; Shinyanga (R): 2,260; Urambo: 36,755. Makadirio haya yanatupatia idadi ya wasemaji wa Kisumbwa kuwa ni 361,111.
Haya ni makadirio yanatokana na utafiti wa Mradi wa Lugha za Tanzania uliofanyika katika miaka 2004-6.
Makadirio haya kwa hakika hayajumuishi wasemaji wa Kisumbwa wanaokaa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, wanaoitwa Wayeke, taz. Munongo and Grevisse (hakuna tarehe), wala sehemu nyingine ambazo hazikuzingatiwa na utafiti wa Mradi wa Lugha za Tanzania (LOT).
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- Dahl, E. 1915. Nyamwesi-Wörterbuch. Hamburg: L. Friederichsen & Co.
- Guthrie, M. 1948 The Classification of Bantu Languages. London: International African Institute.
- Guthrie, M. 1967-71. Comparative Bantu. Vol.1 - 4. London: Gregg.
- Kahigi, K. K. 2005. The Sisumbwa Noun: Its Classes and Derivation. In: Occasional Papers in Linguistics, 1. LOT, Univ. of Dar es Salaam. pp. 117–154.
- Kahigi, Kulikoyela K. 2000. Urefu wa irabu katika Kisumbwa. Katika: Lugha za Tanzania / Languages of Tanzania: studies dedicated to the memory of Prof. Clement Maganga (CNWS publications, no 89), uk.51-65. Kuhaririwa na Kulikoyela K. Kahigi, Yared M. Kihore & Maarten Mous. Leiden: Research School of Asian, African and Amerindian Studies (CNWS), Leiden University.
- Kahigi, Kulikoyela K. 2008. Sumbwa-English-Swahili and English-Sumbwa-Swahili Dictionary. LOT PUBLICATIONS: Lexicon Series, No.11. Languages of Tanzania Project, University of Dar es Salaam, Dar es Salaam.
- Maho, Jouni & Bonny Sands. 2002. The languages of Tanzania: a bibliography. (Orientalia et africana gothoburgensia, no 17.) Göteborg: Acta Universitatis Gothoburgensis. Pp ix, 428. ISBN 91-7346-454-6
- Masele, Balla 2001. The Linguistic History of Sisumbwa, Kisukuma and Kinyamweezi in Bantu Zone F. Tasinifu ya Uzamivu. St. John: Memorial University of Newfoundland.
- Munongo, A.M. and F. Grevisse, n.d. Pages D’Histoire Yeke and Les Yeke.
- Nurse, D. and G. Philippson 1980. The Bantu Languages of East Africa: A Lexicostatistical Survey. Katika: E. Polomé and C. P. Hill, eds. Language in Tanzania. London: O.U.P.
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- lugha ya Kisumbwa kwenye Multitree
- makala za OLAC kuhusu Kisumbwa
- lugha ya Kisumbwa katika Glottolog
- http://www.ethnologue.com/language/suw
- http://www.african.gu.se/tanzania/weblinks.html Ilihifadhiwa 4 Oktoba 2006 kwenye Wayback Machine.
- http://www.linguistics.berkeley.edu/CBOLD/Docs/TLS.html (tovuti hiyo ina msamiati wa Kisumbwa)