Kisiwa cha Kaskazini (New Zealand)
Mandhari
Kisiwa cha Kaskazini (kwa Kiingereza: North Island; kwa Kimaori: Te Ika a Máui) ni kimoja kati ya visiwa vikuu viwili vya New Zealand. Mlangobahari wa Cook unakitenganisha na Kisiwa cha Kusini.
Kisiwa hicho kina eneo la km2 113m729 [1] na wakazi 3,287,600 (Juni 2009). Karibu asilimia 76 za watu wa New Zealand wanaishi katika Kisiwa cha Kaskazini.
Miji kumi na miwili iko katika Kisiwa cha Kaskazini, pamoja na mji mkubwa wa Auckland. Mji mkuu wa Wellington unapatikana kwenye sehemu ya kusini ya kisiwa.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Statistics New Zealand Geography - physical features Archived 30 Novemba 2006 at the Wayback Machine.