Nenda kwa yaliyomo

Kipimo cha Beaufort

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
picha ya data inayoonyesha kiwango cha nguvu ya upepo wa Beaufort katika vitengo vya ukubwa, mafundo, na mita / sekunde.

Kipimo cha Beaufort (ing. Beaufort scale) ni mfumo wa kupima kasi ya upepo. Msingi wake si kipimo kamili cha mwendo wa upepo bali kutazama matokeo ya upepo katika mazingira. Mfumo huu hutumiwa zaidi duniani ulianzshwa mnamo 1805 na MWingereza Francis Beaufort.

Kuna ngazi 12 halafu ngazi ya "sifuri" kama hakuna upepo kabisa.

Ngazi za Beaufort[hariri | hariri chanzo]

Namba ya Beaufort Kasi ya upepo Maelezo Kimo cha mawimbi baharini Dalili kwenye uso wa maji Dalili kwenye nchi kavu Picha
km/h mph kts m/s m ft
0 <1 <1 <1 <0.3 Kimya 0 0 tambarare. Kimya. Moshi hupanda bila kunyoka.
1 1-5 1-3 1-2 0.3-1.5 Mwendo kidogo sana 0.1 0.33 Alama za mawimbi madogo Moshi inanyoka kidogo upande
2 6-11 3-7 3-6 1.5-3.3 Upepezi mwepesi 0.2 0.66 Mawimbi madogo, vichwa kama kioo. Upepo husikika kwenye ngozi, majani yanatoa sauti
3 12-19 8-12 7-10 3.3-5.5 Upepezi 0.6 2 Mawimbi, vichwa vinaanza kuwa vyeupe. Majani na matawi madogo yanaonyesha mwendo mfululizo
4 20-28 13-17 11-15 5.5-8.0 Upepezi kiasi 1 3.3 Mawimbi madogo Vumbi na na vipande vya karatasi vinasukumwa
5 29-38 18-24 16-20 8.0-10.8 Upepo mwepesi 2 6.6 Mawimbi marefu kiasi (zaidi ya mita 1); pofu inaanza kuoekana juu ya mawimbi Matawi ya wastani huonyesha mwendo. Miti midogo huanza kuyugayuga.
6 39-49 25-30 21-26 10.8-13.9 Upepo 3 9.9 Mawimbi makubwa, vichwa vyeupe na pofu kila mahali Matawi makubwa huonyesha mwendo. Mliohusikika kutoka nyaya za simu au umeme. Matumizi ya mwamvuli vigumu.
7 50-61 31-38 27-33 13.9-17.2 Upepo mkali 4 13.1 Mawimbi yanauja juu, pofu inaanza kulea Shina za miti huonyesha mwendo. Kutembea dhidi ya upepo kunahitaji nguvu.
8 62-74 39-46 34-40 17.2-20.7 Dhoruba mwepesi 5.5 18 Mawimbi marefu zaidi, huonyesha machafuko, povu nyingi matawi madogo yanavunjika. Ugumu wa kuendesha magari.
9 75-88 47-54 41-47 20.7-24.5 Dhoruba 7 23 Mawimbi marefu, kimo 6-7 m, povu nyingi sana. Vichwa vya mawimbi huvunjika Matawi ya miti inavunjika, miti midogo inaanza kuanguka.
10 89-102 55-63 48-55 24.5-28.4 Dhoruba kamili 9 29.5 Mawimbi marefu sana, bahari yote huonekana nyeupe. Kuona ni vigumu kutokana pofu nyingi hewani Miti inavunjika, mabati yasiyofungwa vema yanapulizwa mbali, vipande vya lami visivyo imara vinasukumwa.
11 103-117 64-72 56-63 28.4-32.6 Dhoruba kali 11.5 37.7 Mawimbi marefu mno, haiwezekani kuona mbali Uharibifu mwingi wa mimea. Paa za nyumba zinarushwa, vipande vikubwa vya lami iliyokatika pia
12 ≥118 ≥73 ≥64 ≥32.6 Tufani ≥14 ≥46 Mawimbi vya kijitu Uharibifu wa mimea unazidi; madirisha huvunjika, majengo mepesi yanaharibika, magari yanaweza kusukumwa, hatari kutokana na takataka inayorushwa.

Picha[hariri | hariri chanzo]

Other websites[hariri | hariri chanzo]