Kipenda Roho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
"Kipenda Roho"
Wimbo wa Rama Dee
Umetolewa 28 Juni, 2016
Aina ya wimbo R&B/soul
Lugha Kiswahili
Urefu 3:46
Studio Hometown Studio
Mtunzi Nikki wa Pili
Mtayarishaji Elly Dabway
Vankuva
Msafiri
Rama Dee

Kipendacho Roho ni jina la wimbo wa R&B na soul na ballad uliotoka tarehe 28 Juni, 2016 kutoka kwa msanii wa muziki wa R&B na soul kutoka nchini Tanzania, Rama Dee . Wimbo umetungwa na Nikki wa Pili na kutayarishwa kwa ushikiano wa Elly Dabway, Vankuva na Rama Dee mwenyewe. Moja kati ya nyimbo kali za R&B kwa mwaka wa 2016. Rama Dee ameendeleza kuonesha uwezo wake kuimba R&B kwa kiasi cha juu sana. Jinsi alivyoimba huwezi jua kama Kiswahili. Kachukua muundo uleule wa utayarishaji na floo za mbele. Jinsi anavyoshuka na kupanda huku akisindikiza na piano yenye kutia huzuni kupita kiasi. Hadi sasa Rama Dee ndiye msanii pekee kwa Tanzania aliyeweza kuienzi R&B halisi tangu aanze.

Katika wimbo, Rama Dee anamsihi mpenzi wake awe imara na asisikilize maneno ya watu. Katika mapenzi kuna milima na mabonde:
Chombo kwenye maji/ lake jua yake mvua safari tu, Kwenye mvua metope / si ndumba oh

Halafu anapanda juu sana kwa hisia kali sana katika daraja la kiitikio kwa kusema:
Mbele tunaona vita, kipenda roho roho yangu
Nishike mkono kuyapita, kipenda roho roho yangu
Tulishinde lengo lao lao, Lengo lao lao lisitimie.

Rama Dee anajaribu kumweleza mpenzi wake atazame lengo la penzi lao. Ukilitazama na kuelewa nini unachotaka, kamwe huwezi kupotea. Anasema:
Ukitazama malengo haukosei, haupotei kwenye love.

Huu ni mmoja kati ya wimbo mkali wenye video simpo hakuna mfano. Video imeongozwa na Pray G kwa kupitia kampuni ya iPen Media Tanzania. Tangu anaanza hadi anamaliza Rama Dee yupo kwenye piano na mtoto mzuri anayesindikiza milindimo ya sauti ya mahaba. Ucheshi mkali aliounesha malkia katika video hii umezidi kupendezesha. Video ina muundo wa kama black-and-white.

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]