Nenda kwa yaliyomo

Kigalicia

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Ramani ya Galicia katika Hispania mpakani na Ureno
Ramani ya lahaja ndani ya Kigalicia:
ya magharibi (bloque oriental), ya kati (bloque central)
na ya mashariki (bloque oriental)

Kigalicia ("galego") ni lugha ya jimbo la Galicia nchini Hispania. Galicia ni jimbo la Hispania kaskazini ya Ureno na Kigalicia ni karibu na Kireno.

Ni lugha ya Kirumi iliyoanza katika urithi wa Kilatini lugha ya Dola la Roma. Wakati ule eneo liliitwa "Gallaecia" likawa jimbo la Galicia lakini pia kaskazini ya Ureno.

Pamoja na msingi wake wa Kilatini maneno mengi kutoka Kiarabu, Kihispania na Kikelti yaliingia katika Kigalicia.

Wareno na Wagalicia husikizana bila matatizo. Hivyo kuna watu wanaosema ya kuwa Kigalicia ni zaidi kama lahaja ya Kireno.

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]