Kibosnia

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Kibosnia ni moja kati ya lugha za Kislavoni, za jamii ya Lugha za Kihindi-Kiulaya, kinachozungumzwa na watu milioni 2.5 - 3.5, zaidi katika nchi ya Bosnia na Herzegovina.

Ni lugha rasmi ya nchi hiyo pamoja na lugha za Kiserbia na Kikroatia ambazo zinafanana nayo sana, ila ina maneno mengi zaidi ya mkopo kutoka Kiarabu, Kituruki na Kiajemi kwa msingi wa dini ya Kiislamu ya watumiaji wengi.

Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kibosnia kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.