Katumba (Rungwe)
Mandhari
Kwa kata nyingine yenye jina hilo, tazama Katumba (Nsimbo).
Katumba ilikuwa kata ya Wilaya ya Rungwe katika Mkoa wa Mbeya, Tanzania.
Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2002, kata ilikuwa na wakazi wapatao 10,965 waishio humo. [1]
Katumba ni moja kati ya maeneo yanayokua kwa kasi sana. Huko kuna kiwanda cha chai cha Rungwe Tea Growers Association (WAKULIMA). Sasa hivi kuna vijana wengi wanaofanya biashara mbalimbali. Hii imesaidiwa na kwamba Katumba ni mojawapo ya njia panda kuu ya kuelekea Mwakaleli. Njia kuu nyingine ya kuelekea milima ya Kyejo na Masoko ipo Tukuyu mjini. Hivyo basi pamoja na biashara ni sehemu kubwa sana kwa wasafiri wengi wanaoelekea kandokando ya mlima Rungwe na Kyejo.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Repoti Kuu ya Hesabu ya Sensa ya Watu na Makazi kwa Mwaka wa 2002" (kwa Kiingereza). Serikali ya Tanzania. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2004-06-23.
Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Mbeya bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Katumba (Rungwe) kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno. |