Nenda kwa yaliyomo

Katerina wa Medici

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Katerina wa Medici

Katerina wa Medici (Florence, Italia, 13 Aprili 1519 - 5 Januari 1589) alikuwa Malkia wa Ufaransa kama mke wa Mfalme Henri II na mama wa wafalme watatu wa Ufaransa: Francis II, Charles IX, na Henry III[1].

Katerina alijulikana kwa ushawishi wake mkubwa katika siasa za Ufaransa, hasa wakati wa Vita vya Kidini vya Ufaransa. Alijaribu kudumisha mamlaka ya kifalme na kutafuta suluhu za kidiplomasia kati ya Wakatoliki na Waprotestanti (Huguenots). Alishutumiwa kwa jukumu lake katika Machafuko ya usiku wa Mtakatifu Bartholomayo mwaka 1572, ambapo maelfu ya Waprotestanti waliuawa[2].

Katerine wa Medici anakumbukwa pia kwa mchango wake katika sanaa na utamaduni.

Picha ya familia ya Henry na Catherine

Katerina wa Medici aliolewa na Henry, Duke wa Orléans, ambaye baadaye akawa Henry II wa Ufaransa, mjini Marseille mnamo 28 Oktoba 1533. Alizaa watoto kumi, kati yao wanaume wanne na wanawake watatu walifaulu kufikia umri wa ndoa. Watatu wa wake walikuwa wafalme wa Ufaransa, wakati wawili wa wake walioa wafalme na mmoja akawa mke wa Duke. Catherine aliishi zaidi ya watoto wake wote isipokuwa Henry III, ambaye alifariki miezi saba baada yake, na Margaret, aliyeirithi afya yake bora. Victoire na Jeanne walikuwa mapacha waliozaliwa mnamo 1556; Jeanne alizaliwa hajali kutokana na madaktari kuvunja miguu yake kuokoa maisha ya mama yake;[3] Victoire aliishi kwa muda mfupi tu, akifariki chini ya miezi miwili baadaye. Kwa mujibu wa balozi Simon Renard, kuzaliwa kwa mapacha hao karibu kumemuuwa Catherine, na kwa ushauri wa daktari wa Mfalme, wanandoa hao walishauriwa kutokuwa na watoto zaidi.

Louis, Victoire na Jeanne, watoto watatu waliokufa wakiwa wadogo, wakiwa kwenye kitabu cha saa cha Catherine
  • Francis II, Mfalme wa Ufaransa (19 Januari 1544 – 5 Desemba 1560). Alioa Mary, Queen of Scots mnamo mwaka 1558.
  • Elisabeth (2 Aprili 1545 – 3 Oktoba 1568). Aliolewa na Philip II, Mfalme wa Hispania mnamo mwaka 1559.
  • Claude (12 Novemba 1547 – 21 Februari 1575). Alioa Charles III, Duke of Lorraine mnamo mwaka 1559.
  • Louis, Duke wa Orléans (3 Februari 1549 – 24 Oktoba 1550). Alifariki akiwa mtoto mdogo.
  • Charles IX, Mfalme wa Ufaransa (27 Juni 1550 – 30 Mei 1574). Alioa Elizabeth wa Austria mnamo mwaka 1570.
  • Henry III, Mfalme wa Ufaransa (19 Septemba 1551 – 2 Agosti 1589). Alioa Louise of Lorraine mnamo mwaka 1575.
  • Margaret (14 Mei 1553 – 27 Machi 1615). Aliolewa na Henry, Mfalme wa Navarre, baadaye Henry IV of France, mnamo mwaka 1572.
  • Hercules, Duke wa Anjou (18 Machi 1555 – 19 Juni 1584), aliyepewa jina la Francis baada ya kuthibitishwa.
  • Victoire (24 Juni 1556 – 17 Agosti 1556). Alifariki akiwa mtoto mdogo.
  • Jeanne (24 Juni 1556). Alizaliwa hajali.[4]
  1. https://www.britannica.com/biography/Catherine-de-Medici
  2. Hay, Denys, ed., The Letters of James V, HMSO (1954), p. 173, 180–182, 189,
  3. Somervill, Barbara A. (2006). Catherine de Medici. Compass Point Books. uk. 51. ISBN 978-0756515812. Iliwekwa mnamo 12 Juni 2022.{{cite book}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  4. Heritier, 48, inaeleza kwamba vifo vya mapacha hao ni kinyume na haya.
Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Katerina wa Medici kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.