Katapila

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Katapila aina ya Travaux LGV RM500.

Katapila ni gari kubwa aina ya trekta kubwa, litumiwalo katika ujenzi wa barabara, utekuaji miti au uchimbaji.

Ni chombo chenye nguvu na kijiko kipana mbele.

Dreva huketi sehemu iliyonyanyuka ili aone vizuri kazi inavyoendelea.

Magurudumu ni ya chuma au ya mpira na yanakiwezesha kupita sehemu mbaya nje ya barabara.