Kanisa la Kitume la Armenia
Kanisa la Kitume la Armenia (kwa Kiarmenia: Հայ Առաքելական Եկեղեցի), ambalo pengine linaitwa pia Kanisa la Kiorthodoksi la Armenia au Kanisa la Kigregori, ni Kanisa la kitaifa la kale zaidi duniani (301).
Wafuasi wake wanahesabiwa kati ya Waorthodoksi wa Mashariki kwa sababu hawakubali Mtaguso wa Kalsedonia na Mitaguso ya kiekumeni iliyofuata.
Upande wa ibada, linatumia liturujia ya Armenia.
Uongozi na uenezi
[hariri | hariri chanzo]Mkuu wake anaitwa Catholikos (kwa Waarmenia cheo hicho ni cha juu kuliko kile cha "Patriarki") na makao yake makuu yako katika mji wa Echmiadzin, huko Armenia. Kwa sasa ni Karekin II.
Yupo pia Catholikos mwingine mwenye makao makuu Antilyas huko Lebanoni. Kwa sasa ni Aram I.
Kutoka huko wanaongoza Waarmenia milioni 7 hivi waliosambaa duniani hasa baada ya maangamizi ya halaiki yaliyofanywa na Waturuki baada ya Vita Vikuu vya kwanza.
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Catholicosato ya Echmiadzin
- Catholicosato ya Cilicia
- Maktaba pepe ya Kanisa hilo)
- Taarifa kadhaa juu ya Kanisa hilo
- Kitabu cha sala cha Kanisa hilo Archived 25 Februari 2008 at the Wayback Machine.
- Picha za makanisa ya Kiarmenia Archived 29 Agosti 2009 at the Wayback Machine.