Kanada ya Juu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Maeneo ya Kanada ya Juu katika Kanada ya leo.

Kanada ya Juu (Kiing. Province of Upper Canada. Kifar. Province du Haut-Canada) ilikuwa jimbo la kihistoria katika Amerika ya Kaskazini ya Kiingereza (leo Kanada).

Jimbo hili lilianzishwa na Uingereza mnamo 1791 kutokana na maneneo yaliyowahi kuwa sehemu za Jimbo la Quebec.

Jina lilichaguliwa kutokana na mwendo wa Mto Saint Lawrence maana lilikuwa na sehemu za juu za beseni ya mto ilhali Quebec yenyewe ilikuwa na sehemu za chini za beseni hilo.

Kanada ya Juu ilikuwa kimbilio cha watu kutoka sehemu zilizoendelea kuwa Marekani, wakiamua kumfuata mfalme wa Uingereza na kutoshikamana na uasi wa watu wa majimbo ya Marekani dhidi ya mfalme. Sheria na siasa za Kanada ya Juu zilifuata kwa karibu mfano wa Uingereza.

Leo hii sehemu za Kanada ya Juu ya awali zimekuwa sehemu za Jimbo la Ontario katika Kanada.