Kampuni ya Hoteli za Eppley
Kampuni ya Hoteli za Eppley inapatikana katika mji wa Omaha, Nebraska. Wakati wa kununuliwa kwake na Shirika laSheraton katika mwaka wa 1956, ilikuwa ndiyo biashara ya hoteli kubwa kabisa nchini Marekani.
Hoteli ilimilikiwa na tajiri Eugene C. Eppley,kampuni yenyewe ikiwa imeanzishwa katika mwaka wa 1917. Kulikuwa na hoteli 22 katika kampuni hii zilizoenea katika majimbo sita.
Mali zilizomilikiwa
[hariri | hariri chanzo]Hoteli 22 za kampuni hii zilihusu: hoteli iliyo Pittsburgh ya William Penn, hoteli iliyo Louisville,Kentucky ya Seelbach, na ho Hoteli ya 22 katika Eppley Hotel Company's kwingineko included Pittsburgh 's William Penn Hotel, ya Seelbach Hotel katika Louisville, Kentucky na Hotel Fontenelle katika Omaha, Nebraska.
Pamoja na mali nyingine kama hoteli ya West katika Sioux City,Iowa iliyoundwa katika mwaka wa 1903 na ikawa moja ya hoteli za Eppley katika miaka ya 1930. Hoteli hiyo ya West ilichomeka kabisa katika mwaka wa 1953. Hoteli ya Warrior iliyo Sioux City iliundwa chini ya jina la "Hoteli ya Fontenelle" katika mwaka wa 1930. Eppley ilinunua Warrior katika mwaka wa 1936. Kampuni ya Eppley ikauza Warrior kwa Shirika la Sheraton ya Marekani katika mwaka wa 1956. [3]
Hoteli ya Fontenelle ya Omaha ilijengwa katika mwaka wa 1914. Ikiwa pahala maridadi sana,Fontenelle, na ikahudumia wateja maarufu na waliojulikana kama rais wa Marekani,Harry S. Truman na John F. Kennedy. Baada ya kuuzwa na Eppley kwa shirika la Sheraton, hoteli hiyo,Fontenelle, hatimaye ikaanza kuharibika ,ikafungwa katika mwaka wa 1970. Mwishowe,ikabomolewa katika mwaka wa 1983.
Katika mwaka wa 1927, Eppley ilinunua michoro ya rangi ya Grant Woods ya hoteli zake zilizokuwa Council Bluffs,Cedar Rapids,Waterloo na Sioux City. Mchoro wa awali uliochorwa kwa lengo la kuwekwa kwenye chumba cha maakuli cha Hoteli ya Martin, imehifadhiwa katika Kituo cha Sanaa cha Sioux City.
Hoteli za Eppley
[hariri | hariri chanzo]Hoteli zilizokuwa katika kundi la Eppley | |||||
---|---|---|---|---|---|
Jina | Jiji | Maelezo | |||
Hoteli ya Norfolk | Norfolk, Nebraska | ||||
Hoteli ya Lincoln | Lincoln, Nebraska | ||||
Hoteli ya Capital | Lincoln, Nebraska | ||||
Hoteli ya Lindell | Lincoln, Nebraska | ||||
Hoteli ya Fontenelle | Omaha, Nebraska | Ilijengwa katika mwaka wa 1914,hii ndiyo iliyokuwa hoteli bora kabisa katika eneo la Omaha kwa zaidi ya miaka 50.Ilibomolewa katika mwaka wa 1983. | |||
Hotel ya Rome | Omaha, Nebraska | ||||
Hoteli ya Logan | Omaha, Nebraska | ||||
Hoteli ya Cataract | Sioux Falls, South Dakota | ||||
Hoteli ya Carpenter | Sioux Falls, South Dakota | ||||
Hoteli ya Warrior | Sioux City, Iowa | ||||
Hoteli ya Martin | Sioux City, Iowa | ||||
Hoteli ya West | Sioux City, Iowa | ||||
Hoteli ya Tallcorn | Marshalltown, Iowa | ||||
Hoteli ya Chieftain | Council Bluffs, Iowa | ||||
Hoteli ya Montrose | Cedar Rapids, Iowa | ||||
Hoteli ya Magnas | Cedar Rapids, Iowa | ||||
Hoteli ya Seelbach | Louisville, Kentucky | ||||
Hoteli ya Fort Pitt | Pittsburgh, Pennsylvania | ||||
Hoteli ya William Penn | Pittsburgh, Pennsylvania | ||||
Hoteli ya Alexandria | Los Angeles, California | ||||
Hoteli ya Elms Hotel | Excelsior Springs, Missouri |
Muungano
[hariri | hariri chanzo]Eugene Eppley aliiuza kampuni ya Eppley kwa Hoteli za Sheraton katika mwaka wa 1956 kwa bei ya $ milioni 30. Huo ndio uliokuwa bei ghali ya pili katika uuzaji wa hoteli katika historia ya Marekani, wakati huo.
Angalia pia
[hariri | hariri chanzo]Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- "Closing the Gap" Ilihifadhiwa 24 Mei 2009 kwenye Wayback Machine., Time magazine. 4 Juni 1956.
- Take a step back in time: Nebraska Street walking tour Ilihifadhiwa 8 Februari 2008 kwenye Wayback Machine.. Sioux City Museum.
- "Closing the Gap" Ilihifadhiwa 24 Mei 2009 kwenye Wayback Machine., Time magazine. 4 Juni 1956..
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Restaurant Ware Pattern & Other Ephemera Ilihifadhiwa 15 Julai 2011 kwenye Wayback Machine.