Hoteli ya Fontenelle
Hoteli ya Fontenelle ilikuwa hoteli bora ya kibiashara iliyopatikana katika Barabara ya Douglas,katika mji wa Omaha,Nebraska. Ilichorwa na msanifu marufu Thomas Rogers Kimball katika mtindo wa Late Gothic REvival,ikajengwa mwaka wa 1914 na kubomolewa 1983. Iliitwa Logan Fontenelle, mkuu wa kabila ya Omaha aliyejulikana sana.
Kwa miaka mingi, ilikuwa hoteli maarufu sana katika hoteli za kampuni ya Gene Eppley.Katika miaka ya 1950s,kampuni hii ilikuwa kampuni kubwa kabisa ya hoteli iliyomilikiwa na mtu mmoja nchini Marekani.Alikuwa na hoteli 22 katika majimbo sita. Eppley aliishi katika hoteli hiyo baada ya kuinunua katika mwaka wa 1920, na alikufa pale katika mwaka wa 1958. Alikuwa ameuza kampuni yake ya hoteli kwa Shirika la Sheraton kwa bei ya dola milioni thelathini. Hoteli hiyo iliendelea katika operesheni zake katika jina la Sheraton-Fontenelle hadi mwaka wa 1970. Mwaka huo, ilifungwa kwa ghafla kutokana na mabadiliko ya kiuchumi katika mji wa Omaha. Ilibaki tupu hadi wakti ilipobomolewa katika mwaka wa 1983, ikageuzwa kuwa pahala pa kuhifadhi gari. Hivi sasa,ardhi hiyo ni mahakama ya Roman L. Hruska.
Historia
[hariri | hariri chanzo]Fontenelle ilifunguliwa katika mwaka wa 1915. Iligharimu $ 1,000,000 kujenga, jengo lilikuwa limechorwa na kubuniwa na Kimball kwa kampuni ya Hoteli ya Douglas na rais wake,Gurdon W. Wattles. Hapo mwanzoni,ilikuwa na magorofa 15 lakini matatu yakaongezwa yakafika 18,mlango kuu ukiwa kwa Barabara ya Douglas. Jengo hilio lilikuwa na vyumba 350 vya wageni vilivyopambwa kwa mtindo wa Uingereza, sakafu maridadi ya mawe, milango ya mbao gumu,vyumba vya maakuli na kumbi bora bora. Katika chumba kuu cha karamu kulikuwa na mapambo 5 kubwa ya taa na chumba hicho kiliweza kuwa na watu 500 ndani yake.
Ilikuwa ikiendeshwa na Kampuni ya Hoteli ya Douglas hadi mwaka wa 1920, baada ya hapo ikanunuliwa na Eppley. Ikiwa katikati ya jamii ya Omaha , hoteli hii ilikuwa pahala pa matukio nyingi ya raia kama harusi na makongamano, Hasa kuanzishwa kwa Girl Scout katika eneo la Omaha kulifanyika huko, mashindano ya taifa ya bowling ya wanawake ilikuwa pia na mafunzo ya Willa Cather yalihudhuriwa huko pia.
Mikahawa iliyo ndani yake ilikuwa : Bombay Room ,Black Mirror Room na King Cole Room. Hoteli hii iliuzwa katika mwaka wa 1956,ikiwa moja ya hoteli za Eppley, kwa Shirika la Sheraton.Hii ikawa mauzo ya pili kwa ukubwa katika uuzaji wa hoteli za Marekani. Baada ya kununuliwa na Sheraton ,Hoteli ya Fontenelle iliendelea kuwa maarufu kwa kuhudhuria matukio ya kijamii. Hata hivyo, mji ulikua ukielekea upande wa magharibi, hoteli ulianza kupoteza umaarufu na ulifungwa katika mwaka wa 1970. Zaidi ya miaka kumi na tatu zilizofuata, hoteli hiyo ikawa tupu huku watu kadhaa wakitoa maoni kuwa ikarabatiwe ili iwe nzuri. Ilibomolewa katika mwaka wa 1983. [8]
Wageni maarufu
[hariri | hariri chanzo]Watu maarufu na wanasiasa ,kwa miaka mingi, waliishi katika hoteli hiyo.Mmoja akiwa Rais Harry S. Truman aliyekuwa rafiki wa karibu wa Gene Epley. Seneta John F. Kennedy na mke wake Jacqueline akaishi huko wakati wa kampeni yake ya urais katika mwaka wa 1960.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- Gerber, K. and Spencer, J.S. (2003) Architecture for the Ages. Landmarks, Inc. p. 35.(Lugha ya Kiingereza')
- Dalstrom, H.A. (1969) Eugene C. Eppley: His Life and Legacy. Johnsen Press.(Lugha ya Kiingereza')
- Gerber, K. and Spencer, J.S. (2003) Architecture for the Ages. Landmarks, Inc. p. 35.(Lugha ya Kiingereza')
- Historia, Great Plains Girl Scouts Council Ilihifadhiwa 7 Desemba 2008 kwenye Wayback Machine..(Lugha ya Kiingereza')
- Congress, Inc Ilihifadhiwa 24 Mei 2009 kwenye Wayback Machine.. Time magazine. 13 Mei 1936. (Lugha ya Kiingereza')
- 1921 Interview Ilihifadhiwa 21 Agosti 2008 kwenye Wayback Machine.,ChuoKikuu cha Nebraska katika Lincoln.(Lugha ya Kiingereza')
- "Closing the gap" Ilihifadhiwa 24 Mei 2009 kwenye Wayback Machine., Time magazine 4 Juni 1956.(Lugha ya Kiingereza')
- Hoteli ya Fontenelle. (Lugha ya Kiingereza')
- Picha za Maktaba ya Truman Ilihifadhiwa 16 Julai 2011 kwenye Wayback Machine., Maktaba ya Truman
- Dalstrom, H.A. (1969) Eugene C. Eppley: His Life and Legacy. Johnsen Press.(Lugha ya Kiingereza')
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Historic image
- Mchoro wa hoteli ya Fontenelle Ilihifadhiwa 19 Aprili 2012 kwenye Wayback Machine. kutoka kwa Jumba la Kumbukumbu la Durham
- Picha ya nje
- Picha ya ndani
- Picha ya ndani ya chumba cha densi