Kampuni ya Alden
Kampuni ya Viatu ya Alden | |
---|---|
Jina la kampuni | Kampuni ya Viatu ya Alden |
Ilianzishwa | 1884 |
Mwanzilishi | Charles H. Alden |
Huduma zinazowasilishwa | Utengenezaji |
Makao Makuu ya kampuni | Middlesborough, Massachusetts |
Bidhaa zinazosambazwa na kampuni hii | Viatu |
Nchi | Marekani |
Tovuti | Tovuti rasmi ya Kampuni ya Alden |
Kampuni ya Viatu ya Alden ilianzishwa katika mwaka wa 1884 na Charles H. Alden.Hii ni kampuni ya kuunda viatu vya wanaume,vya kazi na vya anasa pia. Kampuni hii ina makao yake Middlesborough, Massachusetts.Hii kampuni ya kuunda viatu ilipatikana katika eneo la New England na inaendelea kuendesha biashara yake huko hadi sasa.
Katika mifululizo ya filamu ya Indiana Jones,Jones huwa amevaa viatu vya aina ya Alden 405 vya rangi ya kahawia. Mwandalizi wa nguo za kuvaliwa katika filamu hiyo, Nadoolman, alikuwa amechagua viatu vya Red Wings kama viatu vya Indy. Viatu vya Red Wings 1905 vinafanana sana na Alden 405, watu hawakuweza kutofautisha viatu hivyo katika filamu za zamani za kabla ya enzi ya DVD(ambazo video huonekana dhahiri zaidi) . Duka ambalo Harrison Ford,anayeigiza kama Indiana Jones(Indy) katika filamu hiyo, alinunua jozi yake ya Alden ya kwanza lilikuwa Duka la Fredrick's Shoes. Fununu ni kuwa Harrison Ford alipendelea viatu vya kampuni ya Alden kwa sababu alivivaa alipokuwa akifanya kazi kama seremala katika jiji la Los Angeles,miaka kadhaa kabla ya kuigiza katika filamu ya Star Wars na kupata umaarufu. Ford, hapo awali,alinunua buti zake katika duka la mtaa wa Sherman Oaks,California lililoendeshwa na Mjerumani aliyeitwa Fritz. Muda ulipokuja wa kununua viatu vingi vya kutumika katika kurekodi kwa filamu ya Raiders of the Lost Ark, Ford alisisitiza kuwa buti zilizohitajika zinunuliwe kutoka duka la Fritz. Timu ya kurekodi na uzalishaji wa filamu wakaheshimu ombi lake.Hivyo basi, Fritz aliuza jozi nyingi za buti katika kurekodi kwa filamu hiyo.Hii inatumika kuonyesha uzuri wa viatu vya kampuni ya Alden na hasa viwango vyake vya juu. Viatu hivyo vya Alden vinajulikana ,pia , kwa sifa ya kudumu sana. Soli na ngozi zake zikiwa dhabiti na bora.
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Tovuti rasmi ya Kampuni ya Alden
- Duka la Alden
- Buti za Jones Ilihifadhiwa 11 Aprili 2011 kwenye Wayback Machine.