Nenda kwa yaliyomo

K. Frimpong

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Alhaji Kwabena Frimpong (alifariki 18 Oktoba, 2005) alikuwa mwimbaji wa nchini Ghana . Alifahamika zaidi kwa wimbo wake wa "Kyenkyen Bi Adi M'awu". [1]

Mnamo miaka ya 1970, alifanya kazi na bendi mbili tofauti. Moja ilikuwa bendi ya Vis-A-Vis, yenye makao yake makuu Kumasi na iliyoongozwa na Isaac Yeboah. Albamu yao ya Obi Agye Me Dofo ilitolewa nchini Ghana katika rekodi lebo ya Probisco, na baadae ilitolewa tena kwenye lebo ya Makossa International. Bendi ya pili ilikuwa Cubano Fiestas, iliyorekodi albamu ya K. Frimpong mnamo 1977 kwa lebo ya Ofori Brothers. Albamu hiyo ilikuwa na wimbo wa "Kyenkyen Bi Adi M'awu" ambao ulimfanya Frimpong afahamike zaidi. Alirekodi tena albamu nyingine mbili na Cubano Fiestas: Me Da A Onnda (1980), na K Frimpong, zote zilitolewa nchini Ghana kwenye rekodi lebo ya Polydor . [2]

Frimpong alifariki tarehe 18 Oktoba, 2005 katika Hospitali ya Komfo Anokye Teaching Hospital, Kumasi, Ghana. [3]

Wanawe wawili wa kiume ni wanamuziki wa rapa wanaoitwa Cabum na Kofi Kapone.

Diskografia

[hariri | hariri chanzo]
  1. "Stylus Magazine: Hiplife". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-12-09. Iliwekwa mnamo 2022-04-23.
  2. Oro, September 2010. Retrieved 18 July 2013
  3. "'Alhaji' K Frimpong Dies", Modern Ghana, 25 October 2005. Retrieved 18 July 2013.
  4. "K. Frimpong & His Cubano Fiestas" at Discogs.
  5. "K. Frimpong* – Okwantuni" at Discogs.