Nenda kwa yaliyomo

Jutland

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rasi ya Jutland

Jutland (Kidenmark: Jylland; Kijerumani: Jütland) ni rasi katika Ulaya ya kaskazini. Sehemu ya kusini ni Ujerumani na sehemu kubwa ya kaskazini ni Denmark.

Mara nyingi ni sehemu ya Denmark pekee inayohesabiwa kuwa Jutland. Kwa maana hiyo Jutland ni sawa na Denmark Bara maana sehemu nyinhine za nchi ni visiwa tu.

Rasi inatenganisha Bahari ya Kaskazini na Bahari ya Baltiki.

Eneo la sehemu ya Denmark ni 29,775 km² ina wakazi 2,491,852 (2004). Karibi karibu yote ni tambarare na vilima vidogovidogo hadi kimo cha 170 m pekee.

Sehemu ya Kijerumani ilikuwa zamani temi mbili za Schleswig na Holstein na siku hizi jimbo la Schleswig-Holstein ndani ya Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani.

Miji mikubwa ya Jutland ni:

  1. Århus, Denmark
  2. Kiel, Ujerumani
  3. Lübeck, Ujerumani
  4. Aalborg, Denmark
  5. Flensburg, Ujerumani
  6. Esbjerg, Denmark
  7. Randers, Denmark
  8. Kolding, Denmark
  9. Vejle, Denmark
  10. Horsens, Denmark

Tazama pia:

[hariri | hariri chanzo]

Historia ya Denmark