Nenda kwa yaliyomo

Judith Patrick Singibala

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Judith Patrick Singibala
Judith Patrick Singibala
Judith Patrick Singibala
Jina la kuzaliwa Judith Patrick Singibala
Alizaliwa 8 Januari 1989
Nchi Tanzana
Kazi yake Mwanaharakati
Tovuti rasmi https://www.tupofoundation.or.tz/

Judith Patrick Singibala (alizaliwa 8 Januari 1989 ) ni mwanamke wa Kitanzania mwanaharakati wa maendeleo ya jamii tanzania. kutokana na kujifunza kutoka kwa wazazi wake. ambao ni waajiriwa katika asasi binafsi, walimpa fursa mbalimbali za kujifunza kutokana na mazingira yao ya ajira.[1]

Alianza kazi katika shirika lisilo la kiserikali kama mkutubi, hali iliyompa motisha na shauku ya kusaidia jamii, hasa zile zenye uhitaji, kwa kuwaunganisha na fursa mbalimbali za kielimu, kibiashara, na kiafya.

Historia yake[hariri | hariri chanzo]

Mnamo mwaka 2012, Judith aliamua kuacha shughuli za ukutubi na kuingia kwenye maendeleo ya jamii. Alipata ajira kama mwalimu wa watoto wenye mahitaji maalum ( special needs teacher). Kwa wakati huo, ilikuwa ni kitu kigeni kwake na kwa jamii kwa ujumla, kwani ilikuwa nadra kukutana na watoto wa aina hiyo. Taratibu, alijifunza na kuzoea mazingira haya mapya yaliyo mkutanisha na watoto wenye upekee wa usonji kitaifa na hata kimataifa. Alikuwa akihudumia watoto 9 kutoka nchi mbalimbali ikiwa ni pamoja na Norway na Uholanzi.[2]

Judith aliendelea kujifunza na kupata ujuzi zaidi kupitia semina, warsha, na mafunzo mbalimbali. Hii ilimsaidia kuimarisha uwezo wake katika kusaidia watoto wenye mahitaji maalum na familia zao. Alianza kushiriki kikamilifu katika miradi ya kijamii, akilenga hasa watoto na vijana waliokuwa wakikosa fursa muhimu za kielimu na kijamii, hasa wenye usonji.

Kupitia kazi yake, amekuwa kiungo muhimu kati ya jamii na fursa zinazopatikana kupitia mashirika yasiyo ya kiserikali na taasisi nyingine za msaada. Kupitia asasi aliyoisajili, wameweza kusaidia familia nyingi kupata elimu bora kwa watoto wao wenye usonji, huduma za afya, na hata fursa za kujiajiri na biashara ndogondogo.

Kwa sasa, Judith anaendelea na kazi zake za kijamii, akilenga kupanua wigo wa msaada kwa jamii nyingi zaidi na kuhakikisha kuwa watoto wote, bila kujali hali zao, wanapata fursa sawa za kuendeleza maisha yao. Ana vipaumbele vikuu vitatu katika kazi zake:

  • Kuwajengea Wanawake Uwezo Judith anawasaidia wanawake kujiamini na kuchangamkia fursa za maendeleo ya biashara na kilimo. Amejiunga na Rural Women Assembly - Tanzania chapter, ambapo anashughulikia masuala ya land advocacy na Gender Based Violence, akitumia psychotherapy kama zana ya kuandaa shughuli zake.
  • Msichana Wangu Project Mradi huu unasaidia mabinti kupata fursa za kujifunza ushonaji, upishi, na elimu ya afya na miili. Kwa sasa, wanahudumia kata ya Kiranyi na shule tatu za msingi, wakitoa taulo za kujisitiri wakati wa hedhi.
  • Watoto Wenye Upekee Judith anasaidia familia za watoto wenye usonji na changamoto nyingine za ulemavu kwa kutoa elimu na zawadi za vitu vinavyothamini haki za binadamu.

Judith anafurahia shukrani kwa elimu aliyopata na kuaminika katika nyadhifa mbalimbali za uongozi katika mashirika binafsi, ambazo zimemjengea uwezo na stahimilivu katika kusaidia walio na uhitaji. Wazazi wake wana mchango mkubwa sana katika kumlea na kumtengeneza kuwa alivyo sasa.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. https://www.linkedin.com/in/judith-singibala-19bb9095/?original_referer=https%3A%2F%2Fwww%2Egoogle%2Ecom%2F&originalSubdomain=tz
  2. "Kuimarisha kujiandaa na kushughulikia dharura za afya ya jamii katika mfumo wa usimamizi wa rasilimali", Usimamizi wa Rasilimali za Miundombinu kwa Maendeleo Endelevu, United Nations, ku. 257–292, 2022-09-29, ISBN 978-92-1-604079-6, iliwekwa mnamo 2024-05-20
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Judith Patrick Singibala kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.