John Saxon

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
John Saxon
Saxon, mnamo 1975
Saxon, mnamo 1975
Jina la kuzaliwa Carmine Orrico
Alizaliwa 5 Agosti 1936
Brooklyn, New York, Marekani
Jina lingine John Saxon
Kazi yake Mwigizaji wa filamu
Miaka ya kazi 1955 mpaka leo
Rafiki Bruce Lee

John Saxon (amezaliwa tar. 5 Agosti 1936) ni mwigizaji wa filamu kutoka nchini Marekani. Saxon pia aliwahi kushiriki katika filamu za western ya Italia, maarufu kama Spaghetti Western, huko alikuwa akicheza kama askari.

Maisha ya Awali[hariri | hariri chanzo]

John Saxon, ni Mtaliano Mmarekani, alizaliwa kama Carmine Orrico mjini Brooklyn, New York, Marekani. John alisomea masomo ya uigizaji, na alifundishwa na moja kati ya wafundishaji maarufu Bi. Stella Adler ni mwanamama maarufu katika masuala ya ufundishaji wa uigizaji nchini Marekani. John alijiingiza katika shughuli za uigzaji mnamo miaka ya 50 hivi, akawa anacheza sehemu za kushiriki kama mtoto.

John Saxon alibahatika kudhaminiwa na bwana Henry Willson, ni baada ya kuona picha ya Saxon katika kasha la gazeti la Dectetive, ndipo bwana Wilson akawasiliana mara moja na familia ya Saxon ilyoko mjini Broklyn, kisha bwana Wilson, kumchukua Saxon na kumpeleka Hollywood, kipindi hicho Saxon alikuwa ana umri wa miaka 16, baadae bwana Wilson akambadilisha jina akamwita Saxon, jina lake la kuzaliwa lilikuwa Carmine Orrico.

Ona pia[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. http://www.filmreference.com/film/25/John-Saxon.html

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]