John McCarthy
Mandhari
'
John McCarthy | |
---|---|
John McCarthy | |
Amezaliwa | Septemba 4, 1927 |
Amefariki | Octoba 24, 2011 |
Kazi yake | mwanasayansi wa kompyuta |
John McCarthy (Septemba 4, 1927 – Octoba 24, 2011) alikuwa mwanasayansi wa kompyuta na sayansi utambuzi wa Marekani. Ni moja kati ya waasisi wa taaluma ya Akili bandia [1].
Alikuwa mwandishi mwenza wa hati iliyobuni neno "Akili bandia", aliunda lugha ya programu ya Lisp, kwa kiasi kikubwa alichangia muundo wa lugha ya ALGOL, alisadia kutangaza ugawanaji-mda na kuvumbua ukusanyaji taka za kielektroniki.
John McCarthy alitumia mda mwingi wa kazi yake kwenye chuo kikuu cha Stanford [2]. Alipokea tuzo za heshima nyingi, kama vile Tuzo ya Turing ya mwaka 1971 kwa michango yake kwenye Akili bandia [3], medali ya taifa ya sayansi ya Marekani na Tuzo ya Kyoto.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "John McCarthy | Biography & Facts | Britannica". www.britannica.com (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2024-01-03.
- ↑ "Professor John McCarthy". jmc.stanford.edu. Iliwekwa mnamo 2024-01-03.
- ↑ "John McCarthy - A.M. Turing Award Laureate". amturing.acm.org. Iliwekwa mnamo 2024-01-03.
Makala hii kuhusu mwanasayansi fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu John McCarthy kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |