Johari (filamu)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Johari
Kasha ya filamu ya Johari.
Kasha ya filamu ya Johari.
Imeongozwa na Vincent Kigosi
Imetungwa na Steven Kanumba
Imetaarishwa na Game First Quality Tanzania
Nyota Steven Kanumba
Blandina Changula
Vincent Kigosi
Mwanaidi Suka
Fadhili Omar
Emmanuel Myamba
Nchi Tanzania
Lugha Kiswahili

Johari I na II ni filamu ya mapenzi na maisha iliyoltolewa mwaka wa 2007 nchini Tanzania.

Muhtasari wa filamu[hariri | hariri chanzo]

Johari (Blandina Changula) na Mainda (Mwanaidi Suka) ni marafiki waliokuwa pamoja na kusoma pamoja, wakiwa shuleni. Kanumba anatokea kumpenda Johari na kumbembeleza awe mpenzi wake ambaye Johari anaona Kanumba hamfai kwani alikuwa anampenda bwana mwingine (Ray-Vincent Kigosi) ambaye alikuwa mtu mkubwa mwenye kazi yake na uwezo pia, bila kutambua kuwa Ray anatumia pesa zake kuwaghilimu wasichana tofauti na kutoka nao kimapenzi ambao wanamuambukiza maradhi ya ukimwi.

Mainda nae anampenda Kanumba ambaye anashindwa kumpa nafasi moyoni kwakuwa Kanumba moyo wake wote ulikuwa umetawaliwa na fikra juu ya kuwa mmoja wa mpenzi wa Johari.

Siku ya siku Johari anagundua maovu ya Ray na kuamua kujinasua kwenye penzi hilo na Ray anamwambia kwa kebehi umeisha Johari kwani anajua alishamuambukiza maradhi ya ukimwi, bila kujua anamkubali Kanumba ambaye hajui kama Johari ameathirika nae kuja kustuka anajikuta ameshaambukizwa akistuka arudi kwa Mainda, Mainda nae keshastuka kuwa Kanumba ameambukizwa kwakuwa anajua miyenendo ya shoga yake.

Johari nae yupo njia panda hajui aolewe na Ray au Kanumba.