Joel Nkaya Bendera

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta

Joel Nkaya Bendera (* 30 Mei 1950 + 6 Desemba 2017) alikuwa mwanasiasa na Mbunge katika Bunge la Tanzania.

Bendera alikuwa kocha msaidizi wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars katika miaka ya 1980 [1].

Aliingia katika siasa kama mbunge wa Korogwe akawa Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo katika serikali ya Mizengo Pinda[2].

Alihudumia kama Mkuu wa Mikoa ya Morogoro na Manyara. Mwezi wa Oktoba 2017 alistaafishwa na rais John Magufuli akaendelea kuwa mbunge wa Tanga hadi kifo chake[3].

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Joel Bendera afariki dunia, Mwanaspoti 6-12-2017
  2. Tanzania National assembly members, Tanzania Foreign Policy and Government Guide, Band 1, uk. 239, iliangaliwa 7-12-2017 kupitia google books
  3. Rais Magufuli atuma salamu za rambirambi kufuatia kifo cha aliyekuwa RC Manyara ‘Joel Bendera’, taarifa ya bongo5.com, 6-12-2017